Tetesi na Usajili Tanzania Bara
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
KLABU ya Young Africans SC imetangaza kukamilisha usajili wa Golikipa, Aboutwaleeb Mshery kutoka Mtibwa Sugar FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Aliyekuwa Kocha msaidizi wa Simba SC, Thierry Hitimana amevunja mkataba wake na klabu ya Simba kama kocha msaidizi baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Golikipa wa Klabu ya Simba SC, Jeremiah Kisubi amejiunga na Mtibwa Sugar kwa mkopo kwaajili ya kuziba nafasi ya Aboutwalib Mshery ambaye amesajiliwa na Young Africans SC.
Klabu ya Simba SC imetajwa kuvunja mkataba na winga wa kiamtaifa wa Malawi Duncan Nyoni Kwa makubaliano ya pande mbili.
Klabu ya Geita Gold FC ya Geita imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Ditram Nchimbi mwenye umri wa miaka 24 kwa mkataba wa mwaka mmoja kutoka Young Africans SC kama Mchezaji huru.
Klabu hiyo pia imekamilisha Usajili wa Beki Juma Said Nyosso mwenye umri wa miaka 37 kwa mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru.
Geita Gold pia imekamilisha Usajili wa Beki wa kulia William Lucian ‘Gallas’ mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru.
Klabu ya Geita Gold imekamilisha Usajili wa beki wa kushoto Adeyun Saleh kutoka Young Africans SC.
Klabu ya Young Africans SC imekamilisha Usajili wa aliyekuwa Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ mwenye umri wa miaka 29 kwa mkataba wa miaka miwili.
Klabu ya Mtibwa Sugar imetangaza kukamilisha usajili wa Mshambuliaji Deo Kanda kutoka DR Congo.
Kabla ya kujiunga na Mtibwa Sugar Kanda amewahi kuzitumikia TP Mazembe, Simba SC, Raja Casablanca, AS Vita Club na DC Motema Pembe.
Klabu ya Geita Gold FC imekamilisha Usajili wa Golikipa Aaron Kalambo kutoka Tanzania Prisons FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Klabu ya Dodoma Jiji FC imemtambulisha mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Mbao FC na Young Africans SC Waziri Junior.
Klabu ya Simba SC ina mpango wa kumsajili Winga Harrison Mwenda raia wa Kenya kutoka Kabwe Warriors ya Zambia.
Klabu ya Young Africans SC ina mpango wa kumsajili mlinzi Abdulmajid Mangalo kutoka Biashara United FC ya Mara Ili kuwapa Changamoto mabeki Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job.
Klabu ya Geita Gold FC imekamilisha Usajili wa aliyekuwa kocha Mkuu wa Biashara United FC Patrick Odhiambo raia wa kenya.
Kocha huyo yupo kwao Kenya tangu alipoachana na Biashara United hivo atarejea Tanzania kwaajili ya kuanza majukumu ya kukinoa kikosi hicho chenye makazi yake Mkoani Geita.
Klabu ya Young Africans SC imekamilisha Usajili wa Kinda Denis Nkane kutoka Biashara United FC ya Mara.
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.
Aliyekuwa beki wa Klabu ya Young Africans SC, Lamine Moro raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 27 anatarajiwa kujiunga na Azam FC.
KLABU ya Simba SC, ina mpango wa kumrejesha kiungo Fraga Vieira raia wa Brazil kwaajili ya kuchukua nafasi ya Taddeo Lwanga raia wa Uganda ambaye ana majeraha ya muda mrefu.
Mgodi wa Uchimbaji madini ya dhahabu wa Geita Gold Mine Limited (GGML) umeingia mkataba rasmi wa udhamini wa klabu ya Geita Gold kwa msimu wa 2021/2022
Mgodi huo umesaini mkataba wa kiasi cha shilingi Milioni miatano (500M) kwa msimu mmoja ikiwa ni katika kuongeza nguvu katika uendeshwaji wa klabu.
Vilabu vya Geita Gold, Mbeya kwanza, Ruvu Shooting, Mtibwa sugar, na Dodoma Jiji vinawania saini ya Mshambuliaji wa Tanzania Prisons Mohammed Mkopi.
Klabu ya Mbeya Kwanza ina mpango wa kumsajili kiungo wa zamani wa Simba SC na Mtibwa Sugar FC, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’
Huenda Klabu ya Simba SC ikasitisha mkataba wa kiungo wa kimataifa wa Uganda Taddeo Lwanga kutokana na majeruhi ya goti ambayo yatamuweka nje kwa zaidi ya miezi mitano.
Klabu ya Young Africans SC bado inaendelea kumsaka mbadala wa mshambuliaji wao Yacouba Songne raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 29 ambaye anatarajiwa kuwa nje kwa msimu mzima wa 2021/2022.
Klabu ya Azam Fc ipo kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa klabu ya Coastal Union Hance Masoud.
Klabu ya Young Africans ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Mcongomani Jean-Marc Mundele Makusu mwenye umri wa miaka 29 kama mbadala wa Yacouba Songne.
Young Africans pia inatajwa kuwania saini ya kiungo wa Kimataifa wa DR Congo Fabrice Ngoma mwenye umri wa miaka 27 kutoka Raja Casablanca ya Morocco.
Klabu ya Coastal Union FC ya Tanga imetajwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa zamani wa Vilabu vya Choma Rangers, Zanaco, Zesco United zote za Zambia, UD Songo ya Msumbiji, Kaizer Chief, Baroka FC na Royal Eagle za Afrika Kusini Lewis Macha raia wa Zambia mwenye umri wa miaka 29.
Klabu ya Geita Gold imeanza mazungumzo na Kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima mwenye umri wa miaka 31 kwaajili ya kumrejesha Tanzania akitokea AS Kigali
Klabu ya Young Africans ipo kwenye mipango ya kuinasa saini ya winga wa TP Mazembe na DR Congo Chico Ushindi katika kuongeza chachu katika kikosi hicho baada ya eneo la winga ya kushoto kukosa mtu sahihi hasa baada ya majeraha aliyoyapata winga Yacouba Songne.
Klabu ya Azam FC imeanza mazungumzo ya kumrudisha mshamabuliaji wake wa zamani Shaban Idd Chilunda.
Klabu ya Young Africans ina mpango wa kumtoa kwa mkopo beki wa kulia Paul Godfrey kwenda Polisi Tanzania FC au Mtibwa Sugar FC.
Klabu ya Young Africans inatajwa kuwania saini ya Mshambuliaji wa Mbeya Kwanza FC, Crispin Ngushi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Tags: NBC Premier League, Tetesi na Usajili Tanzania, tetesi na Usajili Tanzania Bara, Tetesi za Usajili Bongo, Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara, Usajili Bongo, Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara, Usajili NBC Premier League