telegram Nijuze Habari

Tetesi na Usajili Ulaya Leo Ijumaa December 24,2021

Filed in Michezo, Usajili by on 24/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application
Klabu ya Tottenham Hotspur inatathimini uwezekano wa kumnunua beki wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 22. ( via Sun)

Kiungo wa kimataifa wa Uingereza na Arsenal wa chini ya miaka 21 Eddie Nketiah mwenye umri wa miaka 22, anataka kuondoka kwaajili ya kutaka kucheza katika kikosi cha kwanza licha ya Klabu hiyo kutaka kuongeza mkataba wake utakaokamilika msimu ujao wa joto. (Mail)

Klabu ya Juventus inataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial mwenye umri wa miaka 26, na mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang mwenye umri wa miaka 32. (Gazzetta dello Sport, usajili unahitajika)

Meneja wa Tottenham Antonio Conte ameamua kusalia na winga wa Uholanzi Steven Bergwijn mwenye umri wa miaka 24, katika klabu hiyo licha ya vilabu vya ng’ambo kumtaka. (Sky Sports)

Klabu ya Chelsea ina nia ya kumnunua beki wa FC Barcelona na Marekani Sergino Dest mwenye umri wa miaka 21. (El Nacional – via Metro).

Klabu ya Tottenham kwa sasa inaongoza katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie, Klabu hiyo ya kaskazini mwa London italazimika kupambana na Paris St-Germain, ambao pia inamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)

Klabu hiyo pia ina nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Fulham mwenye umri wa miaka 27 kutoka Serbia Aleksandar Mitrovic. (90 Mins)

Kocha Mkuu wa Manchester United, Ralf Rangnick anajiandaa kuwasiliana na klabu yake ya zamani ya RB Leipzig kwaajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Mali Amadou Haidara mwenye umri wa miaka 23, huku akitafuta mbadala wa Nemanja Matic mwenye umri wa 33, raia wa Serbia. (Mirror)

Klabu ya Sevilla imeungana na FC Barcelona katika kinyang’anyiro cha Usajili wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani mwenye umri wa miaka 34. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Klabu ya AC Milan ina matumaini ya kumsajili winga wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech mwenye umri wa miaka 28. (Calciomercato – in Italian)

Klabu ya Liverpool inapania kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Eduardo Camavinga mwenye umri wa miaka 19. (El Nacional – in French)

Klabu ya Newcastle United imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa FC Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele mwenyeumri wa miaka 24, ijapokuwa klabu hiyo ya Uhispania inajaribu kurefusha mkataba wake. (Fabrizio Romano)

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *