Nijuze Habari

Tetesi na Usajili Ulaya Leo Jumatano December 22,2021

Filed in Michezo, Usajili by on 22/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

Klabu za Manchester United, FC Barcelona na Real Madrid zote zinamfuatilia kwa karibu winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman mwenye umri wa miaka 25. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Klabu ya Liverpool imeonesha nia ya kutaka Kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 21 Mnorway Erling Braut Haaland. (Sky Germany)

Klabu ya Everton imekubali mkataba wa pauni milioni 17, kwaajili ya kiungo wa Dynamo Kiev na Ukraine Vitaliy Mykolenko, mwenye umri wa miaka 22, na kupata njia ya kumuondoa mlinzi Mfaransa Lucas Digne mwenye umri wa miaka 28, huku Newcastle na Leicester zikiwa na nia ya kumchukua. (The Mirror)

Mshambuliaji wa kati wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial mwenye umri wa miaka 26, ana mpango wa kujiunga na Sevilla ya Spain kwa mkopo. (Sky Sports)

Klabu ya Manchester United imewasiliana na River Plate kuona kama wanaweza kupata saini ya mshambuliaji Muargentina mwenye umri wa miaka 21 Julian Alvarez, kwa mkataba wa pauni milioni 17 kwa ajili ya .(Ole – in Spanish)

Nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta mwenye umri wa miaka 32, anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya FC Barcelona kuonyesha nia ya kuhitaji saini ya mlinzi huyo Muhispania wakati mkataba wake utakapomalizika msimu huu. (The Athletic – subscription required)

Klabu za Tottenham Hotspur na AS Roma zinagombania sahihi ya kiungo wa kati wa Hoffenheim na Ujerumani Florian Grillitsch, mwenye umri wa miaka 26. (Sky Germany)

Klabu ya Manchester United ina nia ya kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa kati wa Lazio Mserbia Sergei Milinkovic-Savic, mwenye umri wa miaka 26. (Il Messaggero – in Italian)

Klabu ya Chelsea ilitangaza dau la pauni milioni 72 kwaajili ya mlinzi wa Paris St-Germain Marquinhos mwenye umri wa miaka 27, ambalo nyota huyo alilikataa msimu huu. (L’Equipe – in French)

Kiungo huyo Mbrazil Marquinhos anatarajiwa kusaini mkataba mpya katika PSG hadi mwaka 2026 au 2027. (Fabrizio Romano)

Klabu ya Everton itafanya jaribio la tatu la kumsajili kiungo wa Rangers na Uskochi Nathan Patterson mwenye umri wa miaka 20. (Guardian)

Klabu ya Real Madrid inamfuatilia kwa karibu kiungo wa England na Liverpool Joe Gomez mwenye umri wa miaka 24. (Mail)

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.