telegram Nijuze Habari

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa October 21 2022

Filed in Usajili by on 21/10/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa October 21 2022

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa October 21 2022

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa October 21 2022

KLABU za Arsenal, Manchester City, Juventus, Roma na AC Milan wanavutiwa na kiungo wa kati wa Celtic na Jamhuri ya Ireland aliye chini ya umri wa miaka 19 Rocco Vata, 17. (Tuttomercatoweb – in Italian)

Klabu ya Chelsea wako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, kusalia kwa mkopo Inter Milan msimu ujao kabla ya kufutilia mbali mamilioni ya pauni kwa kumuuza. (Gazzetta dello Sport, via Mirror)

Klabu ya Crystal Palace inafikiria kumnunua mshambuliaji wa Blackburn na Chile mwezi Januari Ben Brereton Diaz, 23. (Sun)

Kwengineko, Sevilla wanaongoza Everton, Leeds na Fulham katika mbio za kumsajili Brereton Diaz mwezi Januari (Football Insider)

Klabu ya Arsenal inaweza kujaribu kumsajili beki wa kati wa Ufaransa Evan Ndicka, 23, kutoka Eintracht Frankfurt mwezi Januari. (Standard)

Klabu ya AC Milan inavutiwa na mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 21. (Calciomercato – in Italian)

Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo anakabiliwa na faini ya pauni milioni 1 na klabu hiyo baada ya kutoka nje ya ushindi dhidi ya Tottenham. (Star)

United inaweza kumwachilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kwenda bure mwezi Januari ikiwa hakuna mtu atakayemsajili. (inews)

Klabu za Real Madrid, Paris St-Germain na Manchester City wametuma maskauti kumtazama winga wa Napoli na Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 21.. (90min)

Lakini kiungo wa Slovakia Stanislav Lobotka, 27, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na Napoli, licha ya kunyatiwa na Arsenal, Liverpool na Tottenham. (90min)

Klabu ya Arsenal walikuwa na nia ya kumsajili beki wa Nigeria Calvin Bassey, 22, kutoka Rangers msimu wa joto – kabla ya kuhamia Ajax. (Own Goal Nigeria)

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *