LIVE MBEYA CITY VS YANGA Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 10:00 Jioni.

LIVE SIMBA VS POLISI TANZANIA Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 1:00 Usiku. 

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 19 May 2023

Filed in Michezo, Usajili by on 19/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 19 May 2023

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 19 May 2023

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 19 May 2023

Mshambuliaji wa PSG, Lionel Messi mwenye umri wa miaka 35 amepewa ofa ya €500M/ kwa msimu ili kujiunga na Al Hilal Saudi ya Saudi Arabia.

Al Hilal wanafanya kila iwezekanavyo kuhakikisha wanapata saini ya Mshambuliaji huyo raia wa Argentina, licha ya Familia yake kumtaka kurejea FC Barcelona.

Baada ya kutimuliwa Chelsea, Kocha Graham Potter yupo kwenye mazungumzo ya kina na klabu ya Nice ya Ufaransa ili kuwa Meneja wao mpya, na tayari viongozi wa Klabu hiyo wamekutana mara mbili na Kocha huyo, ambapo amekubali kujiunga nao licha ya kwamba bado hawajafikia Muafaka Rasmi.

Bosi wa Swansea, Russell Martin ni mmoja wa wagombea wanaoongoza kuwa meneja mpya wa Southampton. (Sky Sports)

Winga wa Brighton, Simon Adingra mwenye umri wa miaka 21 anasakwa na vilabu vya Ujerumani na Ufaransa kufuatia kufanya vizuri katika klabu ya Union Saint-Gilloise ya Ubelgiji. ( 90min )

Klabu ya Sunderland iko kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili kiungo wa Birmingham, Jobe Bellingham mwenye umri wa miaka 17, ambaye ni mdogo wa mchezaji wa Borussia Dortmund na kiungo wa kati wa England Jude Bellingham. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa zamani wa Wales, Steve Morison mwenye umri wa miaka 39, anafikiriwa sana kurejea kama meneja wa Cardiff City miezi minane baada ya kufutwa kazi na klabu hiyo. (Wales website)

Manchester United na Newcastle United vimeibuka kuwa vilabu zenye uwezekano mkubwa zaidi wa kumsajili Mshambuliaji wa FC Bayern Munich na Senegal Sadio Mane mwenye umri wa miaka 31, kufuatia kuwa na msimu mbaya wa kwanza nchini Ujerumani. (Mail)

Vilabu vya Chelsea, Manchester United, Tottenham na Fulham ni miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji Mshambuliaji wa KAA Gent, Gift Orban mwenye umri wa miaka 20 kutoka Nigeria. (Evening Standard)

Kipigo cha jumla cha Real Madrid kutoka kwa Manchester City katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa kinaweza kuongeza kasi ya kuondoka kwa bosi wao wa Italia Carlo Ancelotti. (Guardian)

Klabu ya Manchester United inakamilisha mipango yao ya uhamisho wa majira ya kiangazi, huku kiungo wa kati wa Juventus, Adrien Rabiot raia wa Ufaransa mwenye umri wa 28, akirejea kwenye orodha yao walioteuliwa pamoja na mlinzi wa Napoli, Kim Min-jae raia wa Korea Kusini mwenye umri wa miaka 26. (Mirror).

Klabu ya Liverpool inamfuatilia kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Mason Mount mwenye umri wa miaka 24, Pamoja na kiungo wa kati wa Brighton aliyeshinda Kombe la Dunia la Argentina, Alexis Mac Allister mwenye umri wa miaka 24, huku kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch mwenye umri wa miaka 21, akiwa ni mchezaji mwingine anayefuatiliwa na Liverpool. (Liverpool Echo)

Liverpool pia inavutiwa na kiungo wa Feyenoord na Uturuki, Orkun Kokcu mwenye umri wa miaka 22, kama Mbadala wa Mac Allister na kiungo wa kati wa Dortmund, Jude Bellingham mwenye umri wa miaka 19. (Footbal Transfers)

Klabu ya Manchester City, ina nia ya kumsajili beki wa RB Leipzig na Croatia, Josko Gvardiol mwenye umri wa miaka 21, huku klabu hiyo ya Ujerumani ikiomba £85m. (Mail)

Kiungo wa kati wa Chelsea na England, Ruben Loftus-Cheek mwenye umri wa miaka 27, anasakwa na AC Milan ambao wanatazamia kujijenga upya kufuatia kushindwa kwao na Inter Milan katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Fabrizio Romano on Twitter)

Klabu ya Tottenham imeanza Mazungumzo ya kumteua mkufunzi wa Feyenoord, Mholanzi Arne Slot kama meneja wao mpya. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Ecuador, Kendry Paez ameripotiwa kusajiliwa na Chelsea kwa ada ya £20m huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16 pia anaivutia Manchester United. (El Canal del Futbol, via Mirror)

Klabu ya Brentford inatazamiwa kuanza Mazungumzo ya mkataba na Mshambuliaji wa Uingereza, Ivan Toney mwenye umri wa miaka 27, mwishoni mwa msimu huu licha ya kufungiwa kwa miezi minane kutojihusisha na soka kwa makosa ya kamari. (Mail)

Wakati huo huo Brentford, wanataka kumsajili mshambuliaji wa Coventry City na Uswidi, Viktor Gyokeres mwenye umri wa miaka 24 ili kufidia kutokuwepo kwa Toney kwenye timu. (Sport)

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *