TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 26 May 2023

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 26 May 2023

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 26 May 2023
Mshambulizi wa Klabu ya Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 30, amesema kuwa alijua kuwa klabu hiyo ya Italia ingejaribu kumsajili ikiwa uhamisho wake kwenda Chelsea hautafanikiwa. (Mail)
Klabu ya Manchester United inataka kumsajili Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane mwenye umri wa miaka 29, kiungo wa kati wa West Ham, Declan Rice mwenye umri wa miaka 24 na kiungo wa kati wa Chelsea Mason Mount mwenye umri wa miaka 24 pia, msimu huu wa joto. (Sky Sports)
United pia imeanza mazungumzo na mama na wakala wa kiungo wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot mwenye umri wa miaka 28, kwa nia ya kumsajili kwa uhamisho wa bure. (Nicolo Schira)
Klabu ya Tottenham inamfikiria sana Kocha wa Celtic, Ange Postecoglou kama mgombea wa nafasi yake ya umeneja baada ya Arne Slot kuamua kusalia Feyenoord. (Independent)
Spurs pia imewasiliana na meneja wa zamani wa Leicester City, Brendan Rodgers, huku mkufunzi wa zamani wa Chelsea, Graham Potter na kocha mkuu wa zamani wa Uhispania, Luis Enrique pia wakiwa kwenye orodha ya walioteuliwa na klabu hiyo. (Football Transfers)
Hata hivyo, Enrique pia ameibuka kuwa mstari wa mbele kuchukua nafasi ya kocha mkuu wa Paris St-Germain Christophe Galtier. (Goal)
Klabu ya Fulham inajadiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Brazil, Willian ili kuongeza muda wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kusalia Craven Cottage kwa msimu mwingine. (Fabrizio Romano)
Klabu ya Paris St-Germain imewasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Uruguay Manuel Ugarte, huku Chelsea pia ikiwa katika kinyang’anyiro cha kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Fabrizio Romano)

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 26 May 2023
Mshambulizi wa Argentina Angel di Maria anatazamiwa kuondoka Juventus kama mchezaji huru msimu huu wa joto, huku klabu kadhaa za MLS na Saudi Arabia zikitaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35. (90 Min)
Beki wa Ureno Diogo Dalot mwenye umri wa miaka 24, yuko katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na Manchester United. (Fabrizio Romano)
Vilabu vya Newcastle na Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia kiungo wa kati wa Swansea City na Scotland, Azeem Abdulai mwenye umri wa miaka 20. (Mail).
Vilabu vya Chelsea na Liverpool vinamfuatilia kiungo wa kati wa Ubelgiji, Romeo Lavia mwenye umri wa miaka 19, lakini klabu yake ya zamani ya Manchester City haiko mbioni kumsajili kiungo huyo wa kati wa Southampton. (Times – usajili unahitajika)
Klabu ya AC Milan imemfanya kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Ruben Loftus-Cheek, mwenye umri wa miaka 27 kuwa chaguo lao kuu msimu huu. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa Leicester City na Uingereza, James Maddison mwenye umri wa miaka 26, pamoja na mlinzi wa Arsenal na Scotland, Kieran Tierney mwenye umri wa miaka 25, wananyatiwa na Newcastle United msimu huu wa joto huku wakipania kuimarisha kikosi chao kwaajili ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (i Sport)
Qatar Sports Investments, ambayo inaimiliki Klabu ya Paris St-Germain, imefanya harakati za kuwanunua Mabingwa mara nane wa Serie A wa Brazil, Santos. (Mirror)
Klabu ya Aston Villa inaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili winga wa Leicester City, Harvey Barnes mwenye umri wa miaka 25. (Independent)
TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 26 May 2023,Tetesi za usajili ulaya leo 2023,Bbc swahili michezo leo,Tetesi za Usajili Tanzania,Habari za man UNITED za leo,Usajili ulaya man united,Bbc tetesi za usajili,Bbc tetesi za usajili leo Ijumaa May 2023,Bbc tetesi za usajili Leo,Tetesi za usajili barani Ulaya leo Ijumaa, Tetesi za usajili ulaya.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ADA za LIPA kwa Airtel Mitandao Yote
- TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024
- YANGA yashika Nafasi ya 9 Simba ya 10 Afrika 2022/2023
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- Ada zaAirtel Money 2022/2023 | Makato mapya ya Airtel Money
- ADA Mpya za Tigo Pesa (Tigo Pesa Tariffs 2022/2023)
- Ada/Makato ya HaloPesa Tanzania, Halopesa Tariffs 2023
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Bbc swahili michezo leo, Bbc tetesi za usajili, Bbc tetesi za usajili Leo, Bbc tetesi za usajili leo Ijumaa May 2023, Habari za man united za leo, Tetesi za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa, TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa tarehe 26 May 2023, Tetesi za Usajili Tanzania, TETESI ZA USAJILI ULAYA, Tetesi za usajili ulaya leo 2023, Usajili ulaya Man united