Nijuze Habari App

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumanne 14 November 2023

Filed in Usajili, Michezo by on 14/11/2023 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumanne 14 November 2023

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumanne 14 November 2023

Mshambuliaji wa Tottenham na Brazil Richarlison mwenye umri wa 26, na winga wa Manchester United Muingereza Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 23, wanawaniwa na klabu za Ligi Kuu ya Saudia. (Telegraph – usajili unahitajika)

Juventus pia wana hamu ya kumsajili Sancho lakini kwa mkopo huku wakitarajia United kulilipa sehemu ya mshahara wake. (Fabrizio Romano)

Haa hivyo, United hawako tayari kumwachilia Sancho kuondoka katika uhamisho wa Januari . (Football Insider)

Beki wa wa Uingereza Reece James mwenye umri wa miaka 23, anaendelea kujitolea kikamilifu kwa Chelsea licha ya Manchester City na Real Madrid kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (90min)

Wamiliki wa Manchester United wanakataa kukutana na maajenti Kwa kuwa wanaamini kuwa wanajaribu kutafuta wateja kuchukua nafasi ya Erik ten Hag kama meneja. (ESPN)

Kiungo wa Corinthians, raia wa Mbrazil, Gabriel Moscardo mwenye umri wa miaka 18, ambaye ameivutia Arsenal na Barcelona, ​​anasema Chelsea walikuwa na nia ya kumsajili msimu huu wa joto. (Talk sports)

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumanne 14 November 2023Klabu ya Real Madrid imewaongeza kiungo wa Ujerumani Florian Wirtz mwenye umri wa 20, mlinzi wa Uholanzi Jeremie Frimpong mwenye miaka 22, na mshambuliaji wa Nigeria Victor Boniface mwenye umri wa miaka 22, kutoka Bayern Leverkusen kwenye orodha yao fupi ya uhamisho. (Football Transfers)

Klabu ya FC Barcelona bado inapania kumuuza winga wa zamani wa Leeds United Raphinha mwenye umri wa miaka 26, msimu ujao, na wanatumai kuwa kubwa za Ulaya zitaweka dau la kumnunua mshambuliaji huyo raia wa Brazil. (Fichajes – kwa Kihispania)

Real Madrid wako tayari kumuongezea mkataba mlinzi wa Brazil, Eder Militao mwenye umri wa miaka 25 hadi angalau 2028. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)

Brighton wamemleta mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson mwenye umri wa miaka 19, sambamba na wachezaji wengine wanaolipwa pesa nyingi katika klabu hiyo na kandarasi yake mpya ya miaka sita. (Football Insider)

Rais wa Bayern Munich, Herbert Hainer anasema kuwa hawana nia ya kumuuza beki wa Canada Alphonso Davies mwenye umri wa miaka 23, licha ya tetesi kwamba Real Madrid wanamtaka. (90 Min)

Raia wa Croatia na meneja wa zamani wa Marseille, Igor Tudor mwenye umri wa miaka 45, anapendekezwa kuchukua nafasi ya Mfaransa Rudi Garcia mwenye umri wa miaka 59 kama kocha wa Napoli. (Fabrizio Romano)

Beki wa zamani wa Italia mzaliwa wa Naples, Fabio Cannavaro mwenye umri wa miaka 50, pia yuko kwenye orodha ya wale wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Garcia. (Mail)

Chanzo: BBC Swahili

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *