LIVE MBEYA CITY VS YANGA Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 10:00 Jioni.

LIVE SIMBA VS POLISI TANZANIA Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 1:00 Usiku. 

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumanne tarehe 16 May 2023

Filed in Usajili, Michezo by on 16/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumanne tarehe 16 May 2023

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumanne tarehe 16 May 2023

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumanne tarehe 16 May 2023

Klabu ya PSG inamsaka kwa njia yoyote kiungo wa kati wa Ureno an Manchester City, Bernardo Silva mwenye umri wa miaka 28 ili kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi mwenye umri wa miaka 35. (Le Parisien).

Klabu ya Arsenal iko tayari kuipa West Ham United kiasi cha £90m ambayo ni rekodi ya klabu kwaajili ya kiungo wa kati wa England Declan Rice mwenye umri wa miaka 24, wakati Granit Xhaka wa Switzerland mwenye umri wa miaka 30, anaweza kuwa mmoja wa wachezaji watakaouzwa na Klabu hiyo msimu huu wa joto. (Mail)

Kiungo wa kati wa Argentina, Alexis Mac Allister ambaye amekuwa akihusishwa na Vilabu vya Liverpool na Manchester United, anataka kujiunga na klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ataondoka Brighton msimu huu wa joto. (Athletic)

Meneja mpya mtarajiwa wa Chelsea, Mauricio Pochettino anatazamiwa kufanya mazungumzo na Mason Mount ili kumshawishi kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 24 kuongeza mkataba mpya ambao unamalizika msimu wa joto wa 2024. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Wolves, Ruben Neves anasakwa na FC Barcelona, ​​huku Wolves ikitaka angalau pauni milioni 45 ikiwa watamruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuondoka msimu huu wa joto. (Telegraph)

Klabu ya Newcastle United imeongeza kasi ya kumnasa kiungo wa Hungary mwenye umri wa miaka 22, Dominik Szoboszlai ambaye ana kipengele cha kuuzwa kwa euro 70m (£60.9m) katika kandarasi yake ya RB Leipzig, lakini hakuna mawasiliano yoyote yaliyofanyika kati ya vilabu hivyo. (Sky Sports)

Newcastle pia inavutiwa na kiungo wa kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23, Conor Gallagher huku wakitarajiwa kukabiliana na ushindani kutoka kwa Tottenham wanaomtaka mchezaji mwenzake wa kimataifa wa England anayekipiga Leicester City James Maddison. (Mail)

Vilabu vya Bayern Munich na Borussia Dortmund vyote vinamtaka kiungo wa kati wa Mexico Edson Alvarez mwenye umri wa miaka 25, ambaye Ajax Amstadam inaweza kuwa tayari kumuuza kwa £30m. (SPORT1)

Mabeki wa Uingereza Phil Jones mwenye umri wa miaka 31 na Axel Tuanzebe mwenye umri wa miaka 25, wanatarajiwa kuuzwa na Manchester United msimu huu wa joto. (ManchesterEveningNews)

Klabu ya Manchester United inafikiria kumnunua mlinda mlango wa Borussia Dortmund, Gregor Kobel ingawa klabu hiyo ya Ujerumani inakusudia kumpa mkataba mpya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi mwenye umri wa miaka 25. (Independent)

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *