Nijuze Habari

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano August 24,2022

Filed in Usajili by on 24/08/2022 0 Comments

Tetesi za Usajili Ulaya Leo, Tetesi za Usajili Ulaya, Tetesi za Usajili Barani Ulaya, Tetesi za Usajili, Usajili Ulaya, Usajili Ulaya Leo, Usajili Barani Ulaya, Dondoo na Tetesi za Usajili Ulaya, Dondoo za Usajili Ulaya, Habari za Usajili Ulaya, Habari za Usajili Barani Ulaya, Nijuze Habari za Usajili, Nijuze Habari za Michezo, Nijuze Habari Kwenye Usajili, Nijuze Habari za Usajili Ulaya.

Nijuze Habari Application

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano August 24,2022

Tetesi za Usajili Ulaya Leo, Tetesi za Usajili Ulaya, Tetesi za Usajili Barani Ulaya, Tetesi za Usajili, Usajili Ulaya, Usajili Ulaya Leo, Usajili Barani Ulaya, Dondoo na Tetesi za Usajili Ulaya, Dondoo za Usajili Ulaya, Habari za Usajili Ulaya, Habari za Usajili Barani Ulaya, Nijuze Habari za Usajili, Nijuze Habari za Michezo, Nijuze Habari Kwenye Usajili, Nijuze Habari za Usajili Ulaya.

KLABU ya FC Barcelona na Chelsea zote zimeonyesha nia ya kutaka saini ya Harry Maguire, lakini Manchester United wamegoma kumuuza beki huyo wa zamani wa Leicester mwenye umri wa miaka 29 (Chanzo: neil custis)

Klabu ya Chelsea ina mpango wa kumuuza kiungo wao Conor Gallagher mwenye umri wa miaka 23 iwapo itapokea ofa ya takriban £35m (Chanzo: Daily Mail)

Klabu ya Nottingham Forest imeingia kwenye kinyang’anyiro na vilabu vya AC Milan na Napoli katika kusaka saini ya beki wa Japhet Tanganga mwenye umri wa miaka 23 kutoka Tottenham Hotspur.(Chanzo: The Athletic)

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano August 24,2022Everton imeitaka Chelsea kumjumuisha kiungo Conor Gallagher au mshambuliaji Armando Broja kwa mkopo kama sehemu ya mpango wa kumsajili Mshambuliaji wao Anthony Gordon mwenye umri wa miaka 21. (Chanzo: talk SPORT)

Fulham ipo kwenye Mazungumzo ya kina na Klabu ya PSG ili kumsajili beki wa kushoto Layvin Kurzawa raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29.(Chanzo: Sky Italia)

Mshambuliaji Callum Hudson-Odoi mwenye umri wa miaka 21 yuko mbioni kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Bayer Leverkusen ya Ujerumani kutoka Chelsea (Chanzo: Sky Sports)

Klabu ya Manchester United inaweza kuwasilisha ombi la kumnunua Antony mda wowote kuanzia leo, bodi ya Ajax Amstadam imegawanyika kuhusu kumuuza au kutomuuza (Chanzo: Alex crook)

Everton ipo kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu usajili wa James Garner (Chanzo: The Athletic)

Kinda wa Crystal Palace, Luke Plange mwanya umri miaka 19, anatazamiwa kujiunga na klabu ya RWD Molenbeek ya Ubelgiji kwa mkopo wa msimu mzima.
(Chanzo: Mike mcgrath)

Eric Bailly yuko Ufaransa kwaajili ya kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Marseille akitokea Manchester United.
(Chanzo: Mode55489648)

kwa mujibu wa The Athletic wameripoti kuwa Uhamisho wa nyota wa zamani wa Tottenham Dele Alli kwenda Beşiktaş ni suala la muda tu kukamilika akitokea Everton
(Chanzo: The Athletic)

Mshambuliaji Mauro Icardi huenda kujiunga na Klabu ya Galatasaray. (Chanzo: lequipe)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Edinson Cavani yuko mbioni kukamilisha uhamisho wa bila malipo wa kujiunga na na Valencia
(Chanzo: Goal)

West Ham United imewasilisha ofa mpya ya €11m pamoja na nyongeza kwa kiungo Hans Van wa Club Brugge.
(Chanzo: Fabrizio Romano)

Klabu ya Nottingham Forest imekubali mkataba wa pauni milioni 4.2 ili kumsajili mshambuliaji Hwang Ui-Jo kutoka Bordeaux,

Pia Klabu hiyo unafikilia kumpeleka kwa mkopo Olympiacos.(Chanzo: Sky Sports)

Tottenham bado ina nia ya kumsajili winga wa Wolverhampton Wanderers Adama Traore huku Antonio Conte akiataja kuongeza Mshambuliaji mmoja ili kuongeza nguvu Katika safu yake ya Ushambuliaji (Chanzo: Daily Express)

Baada ya kudumu kwa miaka saba ya Oriol Romeu Katika Klabu ya Southampton inaweza kuwa ndio mwisho wa kuendelea klabuni hapo kwani kiungo huyo yuko tayari kukubali kuhamia Girona.(Chanzo: Daily Telegraph)

Juventus ipo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji Arkadiusz Milik kutoka Marseille.(Chanzo: Sky Italia)

Newcastle wamekubali kutoa ada ya pauni milioni 60 ili kumsajili mshambuliaji wa Real Sociedad Alexander Isak.(Chanzo: The Athletic)

West Ham wametuma ofa ya €40m kwa kiungo wa Klabu ya Lyon Lucas Paqueta (Chanzo: Sky Sports)

Klabu ya Nottingham Forest wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa kulia Serge Aurier kwa uhamisho wa bila malipo akitokea Villarreal.(Chanzo: @The Athletic)

Uhamisho wa Nicolas Pépé kwenda Nice kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Arsenal umekamilika, Klabu hiyo ya Ufaransa haitakuwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja.(Chanzo: Lequipe)

Manchester United wameachana na nia yao ya kumnunua Àlvaro Morata baada ya Atletico Madrid kutaka kiasi cha €35m ili kumuuza mshambuliaji wao. (Chanzo: laurie whitwell)

  • USAJILI Uliokamilika Leo Jumatano August 24,2022

Klabu ya Genoa imekamilisha Usajili wa Kevin Strootman kutoka Marseille kwa mkopo wa msimu mmoja, huku kukiwa na chaguo la kumnunua moja kwa moja.

Montpellier imethibitisha kumsajili beki wa kati Christopher Jullien kutoka Celtic kwa ada ya €1m, akisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumika Klabu yake mpya ya Montpellier.

Aris Saloniki amemsajili beki wa kati Nicolas N’Koulou kwa uhamisho bure kutoka Watford.

Klabu ya Valencia imemtambulisha beki wa kati Cenk Özkacar waliemsajili kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Lyon

FC Utrecht imemsajili kiungo Jens Toornstra kwa uhamisho wa bure akitokea Klabu ya Feyenoord.

Klabu ya Troyes imemsajili winga Rony Lopes kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Klabu ya Sevilla.

Golikipa Martin Fraisl amejiunga na Klabu ya Arminia Bielefeld kwa uhamisho bure akitokea Schalke.

Bruno Jordao amejiunga na Santa Clara akitokea Wolves kwa mkopo wa mwaka mmoja

Klabu ya Levante imekamilisha usajili wa kiungo Mohamed Bouldini kutoka Fuenlabrada kwa Ada ya uhamisho wa €3m.

Omonia Nicosia amemsajili kiungo Moreto Cassama kutoka Stade Reims kwa €1.5m.

Klabu ya FC Luzern imemsajili kiungo Max Meyer kwa uhamisho wa bure kutoka Fenerbahce.

Tetesi za Usajili Ulaya Leo, Tetesi za Usajili Ulaya, Tetesi za Usajili Barani Ulaya, Tetesi za Usajili, Usajili Ulaya, Usajili Ulaya Leo, Usajili Barani Ulaya, Dondoo na Tetesi za Usajili Ulaya, Dondoo za Usajili Ulaya, Habari za Usajili Ulaya, Habari za Usajili Barani Ulaya, Nijuze Habari za Usajili, Nijuze Habari za Michezo, Nijuze Habari Kwenye Usajili, Nijuze Habari za Usajili Ulaya.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.