telegram Nijuze Habari

Tetesi za Usajili Ulaya Leo October 26 2022

Filed in Usajili by on 26/10/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano October 26 2022

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano October 26 2022

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano October 26 2022

Klabu ya Leicester City ina nia ya kumsajili Mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco, Zakaria Aboukhlal mwenye umri wa miaka 22 kutoka Toulouse. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Leicester Muingereza James Maddison, 25, na winga wa Bayer Leverkusen ya Ufaransa Moussa Diaby, 23, wanasakwa na Newcastle United katika dirisha la Januari. (Chronicle Live)

Meneja mpya wa Middlesbrough Michael Carrick anasema atatumia “uhusiano” wake na klabu ya zamani ya Manchester United kuleta wachezaji kwa mkopo. (TalkSPORT)

Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim anasema kila mtu katika klabu hiyo “ana ndoto” ya mshambuliaji wa Ureno wa Manchester United Cristiano Ronaldo kurejea katika klabu hiyo, hata hivyo, timu hiyo ya Ureno haiwezi kumudu mshahara wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37. (Football London)

Paris St-Germain wanataka kuongeza mkataba wa Lionel Messi kwa miezi 12 zaidi. Mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 unatarajiwa kumalizika Juni 2023. (Le Parisien)

Bayern Munich wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan mwenye umri wa miaka 32 msimu ujao. (90Min)

Barcelona wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 25, kutoka Wolves, na makubaliano yanaaminika huenda yakaafikiwa mwezi Januari. (Sport)

Chelsea wanamtaka mkuu wa masuala ya usajili wa Brighton Paul Winstanley baada ya kuwaleta wakurugenzi wa kiufundi Laurence Stewart, kutoka Monaco, na Christopher Vivell, aliyekuwa RB Leipzig, pamoja na mkurugenzi mwenza wa zamani wa Southampton Joe Shields. (Guardian)

Manchester United wamefurahishwa na kazi inayofanywa na mkurugenzi wa soka John Murtough huku kukiwa na tetesi kwamba wanakaribia kumteua mkurugenzi wa zamani wa Liverpool Michael Edwards katika nafasi yake. (Express)

Manchester City itapokea 40% ya ada yoyote ya uhamisho iwapo Real Madrid itaamua kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Brahim Diaz, 23 kwenda Manchester United. Kipengele cha ‘anti-United’ kilijumuishwa katika uhamisho wa Diaz wa £15.5m kutoka City kwenda Real mwaka 2019 na bado ni halali. (Gazzetta dello Sport, via Star)

Chaguzi za Ronaldo za kuhamia Marekani ni pamoja na vilabu vya Ligi Kuu ya Soka Inter Miami, LA Galaxy na LAFC. (Los Angeles Times) Arsenal wako tayari kumpa kiungo wa Ubelgiji Albert Sambi Lokonga, 23, kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27. (Calciomercato – in Italian).

Chelsea wana nia ya kuanza mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, 28, baada ya Kombe la Dunia. Mkataba wake wa sasa umebakiza chini ya miaka miwili. (Evening Standard)

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *