TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano tarehe 3 May 2023

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano tarehe 3 May 2023

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano tarehe 3 May 2023
Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi mwenye umri wa miaka 35 ataondoka PSG mwishoni mwa msimu huu baada ya Mabingwa hao wa Ufaransa kuamua kutoongeza mkataba wake. (FootMercato)
Klabu ya Manchester United imeainisha nyota watatu mbadala wa Mshambuliaji wa Tottenham na England, Harry Kane mwenye umri wa miaka 29 endapo watamkosa, Wachezaji hao ni Mchezaji wa Ufaransa wa Eintracht Frankfurt, Randal Kolo Muani mwenye umri wa 24.
Wengine ni Mshambuliaji wa Roma na England, Tammy Abraham mwenye umri wa miaka 25, na mchezaji wa kimataifa wa Argentina, Lautaro Martinez mwenye umri wa miaka 25 kutoka Inter Milan. (FourFourTwo)
Wamiliki wenza wa Chelsea Todd Boehly na Behdad Eghbali walikutana Los Angeles mwishoni mwa wiki iliyopita kujadili uteuzi wa Meneja wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino ili awe Meneja ajaye wa klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Evening Standard)
Mmiliki wa Arsenal Stan Kroenke anatarajiwa kumpa Meneja wa Gunners Mikel Arteta kitita cha pauni milioni 200 ili kuimarisha kikosi chake msimu huu wa joto. (Football transfers)
Klabu ya West Ham imeanza kutafuta Kiungo Mbadala wakijiandaa kumkosa Mchezaji wa kimataifa wa England, Declan Rice mwenye umri wa 24 anayesakwa na Arsenal. (Football Insider)
Klabu ya Tottenham inatarajiwa kupigana vikumbo na mahasimu wao wa London Kaskazini Arsenal katika mbio za kujaribu kumsajili beki wa Crystal Palace na England, Marc Guehi mwenye umri wa miaka 22. (Evening Standard).
Klabu ya Bayern Munich wako tayari kusikiliza ofa kwaajili ya Mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane mwenye umri wa miaka 31 ambaye alijiunga nao akitokea Liverpool msimu uliopita wa joto. (90Min)
Klabu ya Fulham inapanga kufanya mazungumzo na Leeds United kuhusu kumpa mkataba wa kudumu winga Muingereza, Dan James mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)
Mazungumzo ya Tottenham na Meneja wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann kuhusu kuwa Kocha wao mpya yamekwama kwa sababu ya sintofahamu kuhusu nafasi ya Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo. (Telegraph)
Sam Allardyce yuko kwenye Mazungumzo ya kuwa Meneja ajaye wa Leeds United na amepewa bonasi ya pauni milioni 1 ikiwa ataibakisha klabu hiyo ya Elland Road kwenye Ligi kuu England. (Star)
Allardyce atapata bonasi ya zaidi ya £2.5m ikiwa ataweza kuibakisha Ligi Kuu Leeds United na anamtaka Meneja wa zamani wa Oxford United, Karl Robinson kuwa msaidizi wake pale Elland Road. (Times)
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano tarehe 3 May 2023