Nijuze Habari

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatatu June 27,2022

Filed in Usajili by on 27/06/2022 0 Comments

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatatu June 27,2022VILABU vya Villarreal na West Ham United vimefanya mazungumzo juu ya winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma mwenye umri wa 25. (Toni Juanmarti – in Spanish)

Nijuze Habari Application

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatatu June 27,2022

TETESI za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatatu June 27,2022VILABU vya Villarreal na West Ham United vimefanya mazungumzo juu ya winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma mwenye umri wa 25. (Toni Juanmarti – in Spanish)

Imeelezwa kuwa Kocha wa Manchester United Erik ten Hag anaweza kuwa na pauni milioni 100 tu kuijenga upya klabu hiyo msimu huu wa joto. (Sun)

Klabu ya Tottenham Hotspur imeulizia kuhusu beki wa RB Leipzig wa Croatia Josko Gvardiol mwenye umri wa miaka 20. (Nabil Djellit – in French)

Kiungo wa Paris St-Germain, Angel di Maria mwenye umri wa miaka 34, ambaye mkataba wake na Klabu hiyo unamalizika mwishoni mwa mwezi huu, anakaribia kuhamia Juventus, licha ya FC Barcelona kuvitiwa naye. (Calciomercato – in Italian)

Beki wa Manchester United Brandon Williams, mwenye umri wa miaka 21 hana mahitaji ya ziada Old Trafford na anaweza kupatikana kwa £10m msimu huu wa joto. (Mail)

Klabu ya Atletico Madrid inamfuatilia beki wa Celtic wa Croatia Josip Juranovic mwenye umri wa miaka 26. (Record)

Klabu ya Monaco inamwinda mshambuliaji wa Torino na Italia Andrea Belotti mwenye umri wa miaka 28, huku AC Milan pia wakiwa mbioni kumsajili nyota huyo. (Ekrem Konur)

Klabu ya Leeds imewatambua kiungo wa RB Leipzig na Marekani Tyler Adams mwenye umri wa miaka 23 na kiungo wa kati wa RB Salzburg kutoka Mali Mohamed Camara mwenye umri wa miaka 22, kama mbadala wa nyota wa Uingereza Kalvin Phillips mwenye umri wa miaka 26 ambaye anaonekana kukaribia Manchester City. (Mail)

Mshambulizi wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 37, amekataa kujiunga na Inter Miami ya David Beckham hivo atasalia Old Trafford. (Star)

Mshambulizi wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus mwenye umri wa miaka 25 amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na Arsenal. (Guardian)

Klabu ya Liverpool ina uhakika wa kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham(Sun)

West Ham wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse mwenye umri wa miaka 27 msimu huu wa joto. (Sky Sports)

Mchezaji wa Denmark Christian Eriksen anakaribia kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake, huku Tottenham wakiangalia walengwa wengine lakini Brentford wana matumaini ya kumnunua tena mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Fabrizio Romano)

UNAWEZA PIA KUSOMA PIA👇

DOWNLOAD APP MPYA YA NIJUZE HABARI BURE HAPA

UPATE KUTAZAMA MECHI LIVE, MAGAZETI YA KILA SIKU ASUBUHI PAMOJA NA HABARI NYINGINE NYINGI.

TEMBEA NA DUNIA MKONONI MWAKO UKIWA NA APP HII, FURAHIA HABARI NA MATUKIO KILA WAKATI.

Download Bure App mpya ya Nijuze Habari kuweza kuangalia Mpira na utaweza kuona matokeo na ratiba ligi zote kubwa Duniani.

APP HII PIA INAKUSOGEZEA

👉HABARI ZA KITAIFA NA KIMATAIFA
👉HABARI ZA MICHEZO NA USAJILI
👉BREAKING NEWS
👉ELIMU NA AFYA
👉KUTAZAMA MECHI MUBASHARA
👉TAARIFA YA HABARI NA VIPINDI MBALIMBALI
👉MAPENZI NA MAHUSIANO
👉AUDIOS MPYA KILA SIKU
👉BURUDANI
👉MAISHA
👉AJIRA MPYA KILA SIKU
👉GOSPEL
👉MAKALA.

BOFYA 👉👉👉 HAPA KUDOWNLOAD BURE

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.