LIVE MBEYA CITY VS YANGA Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 10:00 Jioni.

LIVE SIMBA VS POLISI TANZANIA Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 1:00 Usiku. 

TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024

Filed in Michezo, Usajili by on 01/06/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024

Coulibaly Wanlo Simba SC

Coulibaly Wanlo Simba SC

Klabu ya Simba inatajwa kuiwinda saini ya beki wa kati, Coulibaly Wanlo mwenye umri wa miaka 31 kutoka ASEC Mimosas ya kwao Ivory Coast.

Aubin Kramo Kouamé Simba SC

Aubin Kramo Kouamé Simba SC

Simba pia inaiwinda saini ya winga, Aubin Kramo Kouamé mwenye umri wa miaka 27 kutoka ASES Mimosas ya Kwao Ivory Coast pia.

Leandre Willy Essomba Onana Simba SC

Leandre Willy Essomba Onana Simba SC

Klabu ya Simba imetajwa kuwa kwenye mazungumzo na Winga Leandre Willy Essomba Onana mwenye umri wa miaka 23 kutoka Rayon Sports ya kwao Rwanda.

Onana ndiye Kinara wa Ufungaji katika Ligi Kuu ya Rwanda (Rwanda Premier League) akiwa na magoli 15 na assist 10.

Hassan Saleh Dilunga Simba SC

Hassan Saleh Dilunga Simba SC

Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wao, Hassan Saleh Dilunga kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mwingine.

TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024, Khanyisa Mayo Yanga SC, Khanyisa Mayo Young Africans, Khanyisa Mayo Cape Town City South Africa

Klabu ya Young Africans SC, ipo kwenye Mazungumzo ya kumsajili Mshambuliaji Khanyisa Mayo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Cape Town City ya Afrika Kusini.

Mayo ndiye Kinara wa Ufungaji Ligi Kuu ya Afrika Kusini (South African Premier Division), akifunga mabao 12 sawa na Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns.

Ranga Chivaviro Yanga SCYoung Africans pia inahusishwa na Mshambuliaji wa Marumo Gallants, Ranga Chivaviro mwenye umri wa miaka 30.

Chivaviro ndiye Kinara wa Ufungaji kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, akiwa na magoli matano (5) sawa na Fiston Mayele wa Yanga SC, huku kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini (South African Premier Division), akiwa na magoli 9 kwenye michezo 17.

Gatoch Panom Yiech Simba SCKlabu ya Simba SC inamnyatia kiungo mkabaji mahiri, Gatoch Panom Yiech raia wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 28 KutokaSt. George SC ya kwao Ethiopia.

Mkataba wa Yiech Panom Gatoch na St. George SC unatajiwa kufikia tamati June 30, 2023.

Fred Felix Minziro Mbeya City FC

Fred Felix Minziro Mbeya City FC

Kocha, Fred Felix Minziro huenda akajiunga na Mbeya City kama Kocha wao Mkuu kuanzia msimu ujao wa 2023/2024 akitokea Geita Gold FC.

Yassin Mustapha Singida Big Stars FC

Yassin Mustapha Singida Big Stars FC

Klabu ya Singida Big Stars FC imepanga kuachana na wachezaji watatu ambao ni beki wa kati Pascal Wawa, Yassin Mustapha na Mshambuliaji Hamis Tambwe mwishoni mwa msimu huu wa 2022/2023.

Paul Nonga Mbeya City FC

Paul Nonga Mbeya City FC

Mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City, Paul Nonga anatarajiwa kuacha kucheza rasmi soka la ushindani mwishoni mwa msimu huu wa 2022/2023.

Baada ya kustafu mpira wa miguu mchezaji huyo atakabidhiwa timu ya vijana ya Mbeya City kama kocha Mkuu.

Gustapha Saimon Coastal Union FC

Gustapha Saimon Coastal Union FC

Vilabu vya Dodoma Jiji, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar vimeonesha nia ya kutaka saini ya nyota Gustapha Saimon kutoka Coastal Union FC.

Gadiel Michael Singida Big Stars FC

Gadiel Michael Singida Big Stars FC

Beki wa Simba, Gadiel Michael na Mshambuliaji Habibu Kyombo wapo Katika hatua za mwisho kutua Singida Big Stars ya Mkoani Singida.

Tuisila Kisinda Yanga SCYoung Africans pia ina mpango wa kuachana na winga wao Tuisila Rossien Kisinda mwenye umri wa miaka 23 kutoka DR Congo mwishoni mwa msimu huu.

Benard Morrison Yanga SCWachezaji wengine ambao Young Africans ina mpango wa kuachana nao kuelekea msimu ujao wa 2023/2024 ni Benard Morrison mwenye umri wa miaka 29, David Bryson, Crysin Ngushi, Dickson Ambundo na golikipa Eric Johora.

Joash Onyango Simba SCBeki wa Kimataifa wa Kenya, Joash Onyango mwenye umri wa miaka 30 ametajwa kuwasilisha barua ya maombi ya kuomba kuondoka katika klabu hiyo aliyoitumikia takribani miaka mitatu.

Nicolas Wakilo Wadada Singida Big Stars FCKLABU ya Singida Big Stars inaidaiwa kukamilisha usajili wa beki wa kulia Nicolas Wadada kutoka Ihefu SC.

Yahya Mbegu Singida Big Stars FC

Huo utakuwa usajili wa pili wa Singida Big Stars baada ya kukamilisha usajili wa beki Yahya Mbegu kutoka Ihefu SC, ambaye alikuwa kwenye rada za Simba SC.

Metacha Mnata Yanga SCUongozi wa klabu ya Young Africans upo kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya wa miaka mitatu (3) golikipa wao Metacha Mnata, baada ya mkataba wa mkopo wa miezi 6 kutoka Singida Big Stars kuisha mwishoni mwa msimu huu.

Denis Nkane Yanga SCWachezaji wengine ambao Young Africans inajadiliana nao kwaajili ya kuongeza mkataba mpya ni Jesus Moloko na Denis Nkane.

Ibrahim Abdallah Hamad Yanga SCBeki wa kati wa Klabu ya Young Africans, Ibrahim Abdallah Hamad amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuwatumikia wananchi kwa miaka mitatu ijayo.

Edmund John Simba SCKlabu ya Simba SC ipo kwenye mazungumzo na kinda wa Geita Gold FC, Edmund John mwenye umri wa miaka 20.

Imeelezwa kuwa Klabu ya Simba ina mpango wa kuachana na Wachezaji wake 11 kuelekea msimu mpya wa 2023/2024.

Wachezaji hao waliotajwa ni Nelson Okwa na Patrick Victor Akpan wote kutoka Nigeria, Augustine Okrah kutoka Ghana, na Mohamed Ouattara kutoka Ivory CoastVictor Akpan, Nassor Kapama and Augustine Okrah Simba SC

Wengine ni Hamed Ismael Sawadogo kutoka Burkina Faso, Peter Banda Kutoka Malawi, Jimmyson Mwanuke, Nassoro Kapama, Beno David Kakolanya, Jonas Gerald Mkude na Gadiel Michael Kamagi wote Watanzania.

Yahya Mbegu Simba SCKlabu ya Simba SC imetajwa kukamilisha Usajili wa beki wa kushoto Yahya Mbegu kutoka Ihefu SC ya Mbeya ili kuziba nafasi ya Gadiel Michael anayeachwa.

Sospeter Bajana and Brno Gomez Simba SCKlabu ya Simba SC ipo kwenye mpango wa kuwasajili viungo, Sospeter Bajana, anayemaliza mkataba wake na Azam msimu huu pamoja na Brno Gomez kutoka Singida Big Stars FC.

Fabien Mutombola and Martin Kizza Simba SCWengine walio kwenye mpango wa Simba SC ni kipa Fabien Mutombola na Mshambuliaji Martin Kizza wote kutoka Vipers ya Uganda.

Benard Morrison Singida Big Stars FC

Benard Morrison Singida Big Stars FC

Klabu ya Singida Big Stars imetajwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha Usajili wa kipa wa Simba SC, Beno Kakolanya, wengine ambao Singida inatajwa kuwinda saini zao ni Benard Morrison kutoka Yanga SC.

Juma Mgunda Simba Sc

Juma Mgunda Simba Sc

Klabu ya Coastal Union ya Tanga ipo kwenye mazungumzo na kocha wao wa zamani, Juma Mgunda ya ili awe kocha wao ajaye kwa msimu ujao wa 2023/2024.

Golikipa nambari mbili wa Simba SC, Beno David Kakolanya amekataa ofa ya kwanza kutoka kwa timu ya kutaka kumuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye makazi yake Mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es salaam.

Beno David Kakolanya Sinba SC

Beno David Kakolanya Sinba SC

Inaelezwa kiwa kipa huyo amepewa ofa ya mshahara wa milioni tano (5m) kwa mwezi pamoja na ada ya usajili milioni 60.

Kakolanya amekataa ofa hiyo na kutoa sababu kuwa anataka kwenda sehemu nyingine ili awe anapata nafasi ya kucheza.

Yassin Mstafa Singida Big Stars FC

Yassin Mstafa Singida Big Stars FC

klabu ya Singida Big Stars huenda ikaachana na beki wake wa pembeni, Yassin Mstafa mwishoni mwa msimu huu, kutokana na ufinyu wa nafasi ndani ya Kikosi hicho cha walima Alizeti.

Yahaya Mbegu Ihefu SC

Yahaya Mbegu Ihefu SC

Kuna uwezekano mkubwa wa beki wa pembeni wa klabu ya Ihefu SC, Yahaya Mbegu kujiunga na Singida BS msimu ujao wa 2003/2024.

Habibu Kyombo Simba Sc

Habibu Kyombo Simba Sc

Singida Big Stars pia  ipo kwenye mazungumzo ya kumrudisha aliyekuwa Mshambuliaji wake, Habibu Kyombo endapo Klabu ya Simba itaamua kumuachia mwishoni mwa msimu huu.

Fred Felix Minziro Geita Gold FC

Fred Felix Minziro Geita Gold FC

Klabu ya Geita Gold ya mkoani Geita huenda ikaachana na Kocha wake Mkuu, Fred Felix Minziro kabla ya msimu huu kumalizika au mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa kutoka ndani ya viunga vya Geita Gold zinasema kuwa Uongozi wa klabu hiyo unafikilia kuachana na Minziro kwa sababu ya kutokuwa na maelewano na wasaidizi wake wa benchi la ufundi.

Thierry Manzi Simba SC

Thierry Manzi Simba SC

Klabu ya Simba imetajwa kumwania beki wa kati na Nahodha Msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda, Thierry Manzi mwenye umri wa miaka 26 kutoka AS Kigali ya kwao Rwanda.

Eric Benjamin Kabwe Simba SC

Eric Benjamin Kabwe Simba SC

Simba pia ipo kwenye Mazungumzo na Mshambuliaji Eric Benjamin Kabwe mwenye umri wa miaka 22 kutoka AS Vita Club ya kwao DR Congo.

Ibrahim Abraham Singida Big Stars FC

Ibrahim Abraham Singida Big Stars FC

Klabu ya Singida Big Stars ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili beki wa kulia wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Ibrahim Abraham.

Arakaza MacArthur Geita Gold FC

Arakaza MacArthur Geita Gold FC

Klabu ya Geita Gold ipo kwenye Mazungumzo ya kumuongezea Mkataba golikipa wao, Arakaza MacArthur raia wa Burundi baada ya kuridhishwa na kiwango chake.

Klabu ya Kitayosce FC ya mkoani Tabora, iliyopanda Ligi Kuu ipo kwenye hatua za mwishoni kukamilisha Usajili wa wachezaji wanne (4) kwaajili ya kusuka kikosi upya kuelekea msimu ujao wa 2023/2024.

Yacouba Sogne & Heritier Makambo Kitayosce FC

Yacouba Sogne & Heritier Makambo Kitayosce FC

Wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na Kitayosce ni Washambuliaji Yacouba Sogne kutoka Ihefu SC, pamoja na Heritier Makambo ambaye hana timu, golikipa Wilbol Maseke Changarawe kutoka Azam FC na Beki Steven Duah kutoka Kagera Sugar.

Crescentius Magori vs Mo Dewji'Mo' Simba SC

Crescentius Magori vs Mo Dewji’Mo’ Simba SC

Inaelezwa kuwa Mdhamini na Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’ amemrejesha kwenye Bodi ya Simba aliyekuwa CEO wa zamani wa timu hiyo Crescentius Magori kwaajili ya kuongeza nguvu ya utendaji kazi ndani ya Bodi hiyo kuanzia Msimu ujao 2023/2024.

Jonas Mkude, Gadiel Michael & Augustine Okrah Singida Big Stars FC

Jonas Mkude, Gadiel Michael & Augustine Okrah Singida Big Stars FC

Wachezaji wanaoondoka Simba SC msimu ujao wa 2023/2024 ni pamoja na Ismail Sawadogo, Augustine Okrah, Gadiel Michael anaenda Singida Big Stars FC, Habibu Kiyombo anaenda Singida Big Stars FC, Jonas Mkude anaenda Singida Big Stars pia, mwingine ni Mohammed Outtara, huku Joash Onyango akiwa 50%/50%.

Mahamoud Mroyvil _ Emery Nimubona Coastal Union FC

Mahamoud Mroyvil _ Emery Nimubona Coastal Union FC

Klabu ya Coastal Union FC ya Tanga imeachana na golikipa wake Mahamoud Mroyvil pamoja na beki wake wa kulia Emery Nimubona raia wa Burundi.

TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024, Tetesi za Usajili Simba 2023,Tetesi za Usajili Tanzania,Usajili NBC 2022/2023, Tetesi za Usajili Yanga 2023,Usajili wa Simba Dirisha Kubwa 2023,Usajili wa Yanga Dirisha Kubwa 2023, Tetesi za Usajili Simba dirisha Kubwa 2023,Tetesi za Usajili Yanga dirisha Kubwa 2023,Tetesi za Usajili Young Africans 2023,Tetesi za Usajili Simba SC 2023,Tetesi za Usajili NBC Premier League Tanzania 2023/2024,Dondoo na tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/2024,Tetesi za Usajili NBC Premier League,Tetesi za Usajili Tanzania 2023/2024 NBC Premier League.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags: , , , , , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *