Nijuze Habari

TETESI za Usajili NBC Premier League August 2022

Filed in Usajili by on 25/08/2022 0 Comments

Tetesi za Usajili Tanzania Bara, Tetesi za Usajili Simba, Tetesi za Usajili Simba SC, Tetesi za Usajili Simba Sports Club, Tetesi za Usajili Yanga SC, Tetesi za Usajili Yanga, Tetesi za Usajili Young Africans SC, Tetesi za Usajili Dar Young Africans, Tetesi za Usajili NBC Premier League, Tetesi za Usajili NBC Premier League 2022/2023, Tetesi za Ligi Kuu Bara, Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara, Tetesi za Usajili, Tetesi za Usajili Tanzania.

Nijuze Habari Application

Lobi Manzoki Simba SC

UONGOZI wa Klabu ya Simba SC umekubali kutoa dau la dola 100,000 (Zaidi ya Milioni 230 za kitanzania) kwaajili ya kukamilisha Usajili wa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Afrika ya Kati Cesar Lobi Manzoki mwenye asili ya DR Congo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Klabu ya Vipers SC ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda.

Aidha mshambuliaji huyo atajiunga na Simba katika dirisha dogo la usajili.

Saido Ntibanzoki Geita Gold FCKlabu ya Geita Gold ya mkoani Geita imekamilisha Usajili wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Young Africans, Said Ntibazonkiza mwenye umri wa miaka 35.

Katibu Mkuu wa Geita Gold FC, Simon Shija amethibitisha kukamilisha usajili Mrundi mwenye mwenye kasi, ambapo amejiunga na Geita kwa mkataba wa miaka miwili.

Saido aliitumikia Young Africans SC kwa muda mwaka mmoja na nusu, akiwa mchezaji muhimu katika kufanikisha Mafanikio waliyopata Yanga kwa kushinda mataji yote msimu uliopita.

Jeremiah Kisubi Polisi Tanzania FCGolikipa wa zamani wa Tanzania Prisons Jeremiah Kisubi amejiunga na Polisi Tanzania akitokea Mtibwa Sugar FC alipokuwa kwa mkopo akitokea Simba SC.

Imeripotiwa kuwa Kisubi amejiunga na Polisi Tanzania kwa uhamisho wa kudumu baada ya kufikia muafaka wa kusitisha mkataba wake na Simba SC.

Victor Patrick Akpan Simba SCUONGOZI wa Klabu ya Simba SC, una mpango kumtoa kwa mkopo Kiungo mkabaji Victor Akpan baada ya Kocha mkuu Zoran Maki kutoridhishwa na Kiwango chake.

Zoran pia ameishauri Simba  kumtoa kwa mkopo Kiungo kiraka Nassoro Kapama kwa kuwa hayuko kwenye mipango yake msimu huu wa 2022/20203.Nassor Kapama Simba SC

Kapama alitua Simba SC miezi miwili iliyopita akitokea Kagera Sugar ya Bukoba, Kagera.

Aliyekuwa Kiungo wa Azam FC, Mdathiri Yahya na Kiungo wa zamani wa Klabu hiyo, Gerson Fraga mmojapo anatajwa kuchukuwa nafasi ya Victor Akpan pale Lunyasi.Gerson Fraga & Mudathir Yahya Abbas Simba SC

Vilabu vya Geita Gold na Coastal Union vimeonesha nia ya kumtaka Victor Akpan kwa mkopo na vinasubiria tamko la Simba SC.

Klabu ya Simba SC imetajwa kukamilisha Usajili wa Kiungo mkabaji, Morice Ugochukwu Chukwu mwenye umri wa miaka 27 kutoka Rivers United ya kwao Nigeria.Morice Ugochukwu Chukwu Simba SC

Kabla ya kusajiliwa Rivers United Chukwu amewahi kuitumikia Klabu ya Akwa Sport Nigeria pia.

Wachezaji wawili wa ndani akiwepo Nassor Kapama watapelekewa kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili kufungwa August 31,2022.

Klabu ya Yanga inaangalia uwezekano ya kumbadilisha Mshambuliaji wake Lazarous Kambole kwenye Usajili wa ndani na abaki kwenye usajili wa kimataifa tu.Lazarous Kambole Yanga SC

Yanga wamefikia uamuzi huo huo baada ya kumuona Kambole kuwa na majeraha ya mara kwa mara.

Pia Yanga ipo kwenye mpango wa kufanya Usajili wa Mchezaji mpya wa Kimataifa na klabu hiyo itakuwa na jumla ya Wachezaji 14 wa Kimataifa huku Wachezaji wawili ambao ni Yacouba Sogne na Kambole kuwatoa listi ya Wachezaji wa Ligi ya ndani na kuwatumia Kwenye Mechi za Kimataifa tu.Lazarous Kambole & Yacouba Sogne Yanga SC

Nahodha wa Klabu ya Simba SC, John Bocco yupo mbioni kuondoka Klabuni hapo kabla ya dirisha la Usajili kufungwa August 31,2022 kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.John Bocco Simba SC

Ramadhan Kabwili Rayon Sports FCKatika hatua nyingine, Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda imekamilisha Usajili wa golikipa wa zamani wa klabu ya Yanga SC, Ramadhan Kabwili kwa mkataba wa mwaka mmoja.Ramadhan Kabwili Rayon Sports FC

Baada ya Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally kuthibitisha kuwa kiungo Mshambuliaji wao Hassan Dilunga hatokuwa sehemu ya kikosi chao msimu mpya wa 2022/2023, uongozi wa Klabu hiyo kupitia kwa Salim Abdallah ‘Try Again’ umesema kuwa Dilunga kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa Simba.

Hassan Saleh Dilunga Simba SC

Try Again ameongeza kuwa Simba SC itaendelea naye mpaka dirisha dogo la Usajili kwaajili ya kuona hali yake, kama atakuwa amepona bado anahitajika sana na mchango wake wanauthamini.

Na aliyekuwa Kiungo Mshambuliaji wa Yanga SC, Chico Ushindi Wakubanza amejiunga na Klabu ya Al-Khums ya nchini Libya mkataba wa mwaka mmoja akitokea TP Mazembe ya Kwao DRC Congo.

Chico Ushindi wa Kubanza Yanga SC

Aidha Dirisha la Usajili la kimataifa la CAF limefungwa rasmi Jana Jumatatu saa 23:59 usiku, huku Dirisha la Usajili wa ndani la Tanzania (TFF) likiwa wazi na linatarajiwa kufungwa rasmi August 31,2022 saa 23:59 Usiku.

Juma Liuzio Geita Gold FCMashambuliaji wa zamani wa mtibwa Sugar Juma Liuzio amejiunga na Geita Gold FC ya Geita kutoka klabu ya Mbeya City ya Mbeya.

Tetesi za Usajili Tanzania Bara, Tetesi za Usajili Simba, Tetesi za Usajili Simba SC, Tetesi za Usajili Simba Sports Club, Tetesi za Usajili Yanga SC, Tetesi za Usajili Yanga, Tetesi za Usajili Young Africans SC, Tetesi za Usajili Dar Young Africans, Tetesi za Usajili NBC Premier League, Tetesi za Usajili NBC Premier League 2022/2023, Tetesi za Ligi Kuu Bara, Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara, Tetesi za Usajili, Tetesi za Usajili Tanzania.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.