Nijuze Habari

TETESI za Usajili Simba na Yanga June 18,2022

Filed in Usajili by on 18/06/2022 0 Comments

Victor Patrick Akpan Simba SCKLABU ya Simba SC imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo Victor Patrick Akpan raia Nigeria mwenye umri wa miaka 23 kutoka Coastal Union ya Tanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Nijuze Habari Application

TETESI za Usajili Simba na Yanga June 18,2022

Victor Patrick Akpan Simba SCKLABU ya Simba SC imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo Victor Patrick Akpan raia Nigeria mwenye umri wa miaka 23 kutoka Coastal Union ya Tanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Klabu hiyo pia imetajwa kukamilisha Usajili wa Kiungo mshambuliaji wa Coastal Union FC pia, Abdul Seleman “Sopu” kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru.Abdul Seleman "Sopu" Simba SC

“Sopu” ni kama anarejea nyumbani kwani alilelewa kwenye timu ya vijana ya Simba B, kabla ya kutolewa kwa mkopo na baadae kusajiliwa moja kwa moja na Coastal Union FC.

Katika hatua nyingine, mshambuliaji anayenyatiwa na Simba SC kutoka Vipers SC ya Uganda ambao ndio Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda Ceser Manzoki, ameteka vyombo vya habari nchini humo, baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo muhimu za Ligi Kuu ya chini humo.Ceser Manzoki Simba SC

Manzoki anayemaliza mkataba wake na klabu ya Vipers SC, alikuwa na msimu mzuri na kufanikiwa kuibeba klabu hiyo hadi kutwaa taji la Uganda msimu huu wa 2021/2022.

Mshambuliaji huyo raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, jana Ijumaa ya June 17,2022 ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo 6 ambazo ni Mchezaji bora wa msimu, Mchezaji bora wa wachezaji, Mshambuliaji bora wa msimu, Mtoa assists bora wa msimu, Kinara wa mabao wa msimu na ametajwa katika kikosi bora cha msimu huu 2021/2022.Ceser Manzoki Simba SC

Mafanikio hayo yanatajwa kuendelea kuitamanisha Simba SC ambayo inatajwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili mshanbuliaji huyo mzaliwa wa DR Congo.

Simba pia inatajwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Augustine Okrah mwenye umri wa miaka 28 kutoka klabu ya Bechem United inayoshiriki Ligi Kuu ya GhanaAugustine Okrah Simba SC

Nyota huyo aliyepachika mabao 14 kwenye Ligi Kuu ya Ghana msimu huu wa 2021/2022 anatarajiwa kujiunga na Simba baada ya msimu kukamilizika na kulingana na mwanahabari huu Nuhu Adams, Okrah atasaini mkataba wa miaka miwili.Moses Phiri Simba SC

Klabu hiyo imejipanga kuboresha safu yake ya ushambuliaji ikiwa tayari imemsajili Mshambuliaji Moses Phiri mwenye umri wa miaka 29 kutoka klabu ya Zanaco FC ya kwao Zambia.

Lazarous Kambole Yanga SC Baada ya kumtambulisha mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka klabu ya Kaizer Chiefs, Uongozi wa Klabu ya Young Africans umesema kuwa bado kuna wachezaji wengine watatu wanasubiri utambulisho.

Stephane Aziz Ki Yanga SCMakamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said amesema mpaka kufikia mwisho wa mwezi huu watawatambulisha nyota wote wa kigeni waliowasajili na Klabu hiyo kwaajili ya msimu ujao wa 2022/2023.Jocye Lomalissa Mutambala Yanga SC

Nyota wanaotajwa kusajiliwa na Young Africans SC ni pamoja na kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas Stephane Aziz Ki, mlinzi wa kushoto Mcongomani Jocye Lomalissa Mutambala kutoka Sagrada Esperanca ya Angola na winga Bernard Morrison aliyemaliza mkataba wake na Simba SC.Bernard Morrison Yanga SC

Kiungo Mshambuliaji wa Tanzania Simon Msuva, amethibitisha kufuatwa na viongozi wa klabu za Simba SC na Young Africans SC, kwaajili ya kuitumikia Klabu mojawapo msimu ujao wa 2022/2023Simon Msuva Wydad Casablanca

Msuva ambaye kwa sasa ni mchezaji huru kufuatia kuachana na Mabingwa wa Soka Barani Afrika upande wa vilabu Wydad Casablanca ya Morocco, yupo nchini kwa zaidi ya miezi mitatu akifanya mazoezi binafsi ya kujiweka fiti.

Simon Msuva Wydad CasablancaKiungo huyo za zamani wa Young Africans SC amesema kuwa huenda akakubali kujiunga na moja ya timu hizo hivyo amewataka Mashabiki wa soka nchini kuendelea kuwa na subra na atatangaza mara baada ya kesi yake kufikia hukumu FIFA dhidi ya klabu yake Wydad Casablanca.

Ibrahim Ame Mohamed Simba SCInatajwa kuwa beki wa kati wa Klabu ya Simba SC, Ibrahim Ame anayecheza kwa mkopo Mtibwa Sugar FC ya Morogoro amegoma kuongeza mkataba huku ikielezwa kuwa ana mpango wa kurejea Coastal Union FC ya Tanga.

Ame alijiunga na Simba SC msimu wa 2020/2021 akitokea Coastal Union FC na kusaini mkataba wa miaka miwili ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa 2021/2022.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.