Nijuze Habari

TETESI za Usajili Tanzania Bara 2022/2023 June 05,2022

Filed in Usajili by on 05/06/2022 0 Comments

Kwame Peprah Simba SCIMEELEZWA kuwa Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameweka Sh 800Mil kwaajili ya Usajili wa msimu ujao 2022/2023 na zimeanza na mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Kwame Peprah, raia wa Ghana.

Nijuze Habari Application

TETESI za Usajili Tanzania Bara 2022/2023 June 05,2022

Kwame Peprah Simba SCIMEELEZWA kuwa Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameweka Sh 800Mil kwaajili ya Usajili wa msimu ujao 2022/2023 na zimeanza na mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Kwame Peprah, raia wa Ghana.

Aidha Klabu hiyo imekuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na Mghana huyo ambaye inaelezwa mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Imeelezwa kuwa Simba SC imepanga kukiimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao baada ya kuonekana kutokuwa na timu imara na bora na kusababisha kupoteza makombe yote waliyokuwa wakiyatetea ambayo ni Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) msimu huu wa 2021/2022.

Stephane Aziz Ki Yanga SCKatika hatua nyingine imeelezwa kuwa Klabu ya Simba SC imeacha na mpango wa kuwania saini ya mshambuiliaji wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast raia wa Burkana Faso, Aziz Ki anayewindwa na Young Africans katika usajili wa msimu ujao 2022/2023.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kuwa klabu hiyo imepanga kufanya Usajili wa Wachezaji wenye hadhi ya juu Barani Afrika kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

Ahmed Ally Simba SCAhmed Ally amesema kuwa Simba SC imedhamiria kufanya Usajili mkubwa msimu ujao, na wachezaji watakaopewa kipaumbele ni wale walioziwezesha klabu zao kufika hatua ya Robo Fainali katika michuano ya Kimataifa msimu huu.

Ahmed Ally Simba ameongeza kuwa baadhi ya wachezaji wataachwa na wengine wataendelea kuwa sehemu ya timu hiyo, watakaosajiliwa wataungana na watakaowakuta ili kuunda timu ambayo tunaamini itakua imara kwa michuano ya ndani na nje ya Tanzania.

Pascal Wawa Simba SCWachezaji ambao wanaweza wasiongezwe mikataba ni pamoja na Paschal Wawa, Meddie Kagere, Chris Mugalu na Taddeo Lwanga huku Bernard Morrison akiwa tayari amepewa mkono wa kwa heri.

Jimmyson Mwanuke Simba SCJimmyson Mwanuke na Yusufu Mhilu wanatajwa kuwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo wakati Larry Bwalya anaweza kuuzwa kwenye klabu moja huko Afrika Kusini.

Pablo Franco Martin Simba SCWakati huo huo Simba imeendelea kupokea CV za makocha mbalimbali ambao wanawania kumrithi Pablo Franco aliyetimuliwa karibuni.

Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara amesema kuwa klabu hiyo itafanya Usajili mkubwa utakaozingatia ripoti ya Benchi la Ufundi.

Young Africans imepanga kufanya usajili huo, huku ikiwa klabu pekee msimu huu 2021/2022, iliyoonyesha kuwa na kikosi imara ambacho hakijapoteza mchezo hata mmoja wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Haji Manara Simba SCManara amesema klabu hiyo ina malengo makubwa kuelekea msimu ujao, hasa ikizingatiwa itashiriki Michuano mikubwa Barani Afrika, hivyo watahakikisha wanapata wachezaji wenye hadhi ya juu.

Amesema pamoja na kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kupambana msimu huu, bado Uongozi unaamini ripoti ya Kocha Mohamed Nabi itatoa mapendekezo ya usajili ambayo lazima yatafanyiwa kazi kwa asilimia 100.

Saido Ntibazonkiza Yanga SCHadi sasa Tetesi zinaeleza kuwa Young Afrcans huenda ikawaacha wachezaji zaidi ya 10 mwishoni mwa msimu huu, huku ikiwa tayari imeshaachana na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza, baada ya kumaliza mkataba wake, pia alihusishwa na utovu wa nidhamu wakati timu ilipoweka Kambi jijini Mwanza kwa maandalizi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC”.

Lazarous Kambole Yanga SCKlabu ya Young Africans ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa Mzambia, Lazarous Kambole, anayekipiga Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini kwaajili ya kukiimarisha Kikosi chake kuelekea Michuano ya kimataifa Mssimu ujao 2022/2023.

Bernard Morrison Yanga SCKlabu hiyo pia ipo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji wengine wa kigeni akiwemo Mghana, Bernard Morrison aliyemaliza mkataba wake Simba SC.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba Salim Abdallah ‘Try Again’ amefunguka mengi juu ya timu hiyo na kwamba itarudi kwenye levo zake kwa kishindo.

Try Again anasema; “Tunarudi kwa kishindo, tunarudi kwa kishindo. Nimezungumza na mwekezaji wetu MO Dewji kuwa atasajili (wachezaji).

Salim Abdallah ‘Try Again’ Simba SC“Tutawekeza kwenye miundombinu, kikubwa tunaomba wapenzi wa Simba tumpe ushirikiano, lakini tunawaahidi tutarudi kwa kishindo.

“Sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kikosi, tunasajili vizuri, tutabaki na wachezaji wazuri, kuna wengine umri umekwenda na viwango vimeshuka, lakini hatutawaacha vibaya…Tunawashukuru sana wachezaji na benchi la ufundi.

Mfanyabiashara na mwekezaji wa Simba SC, bilionea Mohamed Dewji (Mo Dewji) amesema kuwa wanaisafisha klabu hiyo kila sehemu inayostahili kufanyiwa hivyo.
“Tunasafisha kila sehemu ambayo inahitaji kuwekwa sawa ili turudi kwenye ubora wetu,” ameeleza hayo  Mo Dewji June 03,2022 kwenye ukurasa wake wa Twitter.

David Etop Udoh Simba SCKlabu ya Simba SC imepanga kumsajili kiungo David Etop Udoh raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 22 kwaajili ya kuchukua nafasi ya Tadeo Lwanga ambaye anatarajiwa kuachana na Klabu hiyo.

Thadeo Lwanga Simba SCKiungo huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 28 ataachana na Simba SC baada ya mkataba wake wa miaka miwili (2) na Klabu hiyo kufikia kikomo msimu huu wa 2021/2022 na Simba hawana mpango wa kumuongezea mkataba mpya.

David Etop Udoh Simba SCKutokana na ukomo wa idadi wachezaji wa kigeni Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba haikuweza kumsajili Udoh ambaye mwanzoni mwa msimu huu alifanikiwa kufanya majaribio Klabuni na kufanya vizuri kwenye Mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2021/2022.

Nathan Fasika Idumba Simba SCKlabu ya Simba SC imeanza mazungumzo na beki wa kati wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Fasika Idumba raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 23 kwaajili ya kuwatumikia wanamsimbazi hao msimu ujao wa 2022/2023

Nathan Fasika Idumba Simba SCIdumba aliyetua Cape Town kutokea FC Saint Eloi ya kwao DR Congo, anatajwa kuja kuwa pacha wa Henock Inonga Baka katika eneo la ulinzi kwa msimu ujao ambapo awali wachezaji hao wamewahi kucheza pamoja.

Nathan Fasika Idumba Simba SCInaelezwa kuwa Simba ina mpango wa kuachana na beki Muivory Coast Pascal Wawa na Erasto Nyoni ambao ni wachezaji wakongwe wa eneo la ulinzi kikosini hapo.

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limewaagiza Wanachama wake kuwasilisha majina ya timu pamoja na wachezaji waliosajiliwa kwaajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika kabla ya June 30,2022.

CAFTaarifa ya CAF imebainisha kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya June 30, 2022.

Fiston Kalala Mayele Yanga SCMshambuliaji wa Young Africans SC, Fiston Kalala Mayele anahusishwa na mpango wa kuachana na klabu hiyo, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kisoka na kuzifumania nyavu za timu pinzani.

Mayele ambaye amefunga zaidi ya mabao 10 katika ligi hiyo, anahusishwa na mpango wa kuwaniwa na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika RS Berkane, chini ya Kocha Mkuu Florent Ibenge.

Fiston Kalala Mayele Yanga SCKwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari kutoka Congo DR vimethibitisha kuwa, Kocha Ibenge ambaye aliwahi kufanya kazi na Mayele katika klabu ya AS Vita, amevutiwa na uwezo wa Mshambuliaji huyo baada ya kumfuatilia kwa ukaribu akiwa Young Africans msimu huu 2021/2022.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imeanza kupokea maoni ya maboresho ya kanuni za Ligi kwaajili ya msimu ujao 2022/2023.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania BaraKwa mujibu wa mtandao rasmi wa Instagram na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) na wa Bodi, wamewataka wadau wote wa soka kutuma maoni kuhusu maboresho ya kanuni ili kuifanya Ligi Kuu Tanzania Bara kuwa bora zaidi.

Mdau anayetaka kutoa mapendekezo ya maoni yake, au maboresho anatakiwa kutuma kwa barua pepe ‘[email protected].’

“Kanuni bora na rafiki huzaa Ligi bora.” ilimalizia taarifa hiyo ya Bodi ya Ligi.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.