Nijuze Habari

TETESI za Usajili Tanzania Bara 2022/2023

Filed in Michezo by on 26/05/2022 0 Comments

KLABU ya Simba SC imetajwa kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji, Cesar Lobi Manzoki kutoka klabu ya Vipers SC ya Uganda.

Nijuze Habari Application

TETESI za Usajili Tanzania Bara 2022/2023

KLABU ya Simba SC imetajwa kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji, Cesar Lobi Manzoki kutoka klabu ya Vipers SC ya Uganda.

Cesar Lobi Manzoki Simba SCMonzoki raia wa Afrika ya kati mwenye asili ya DR Congo akiwa na Umri wa miaka 25 msimu huu wa 2021/2022 amefunga mabao 18 katika Michezo 26 na kuisaidia Vipers kuwa mabingwa wa Uganda na atajiunga kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha mwisho wa msimu huu.

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana, Bernard Morrison (BM3) mwenye umri wa miaka 29 ameweka wazi mpango wake wa kutangaza timu yake mpya atakayoitumikia msimu ujao wa 2022/2023, hii ni baada ya kupewa mapumziko ya hadi mwisho wa msimu na Simba SC.

Bernard Morrison Simba SCKupitia ukurasa wake wa Instagram, kiungo huyo ameweka wazi mpango huo kwa kuandika ujumbe unasomeka “Tafadhali gusa link iliyopo kwenye bio yangu, jisajili kwenye channel yangu na subiri live video kwenye Youtube kujua kituo kinachofuata”.

Mshambuliaji Moses Phiri raia wa Zambia ambaye ametajwa kukamilisha taratibu zote za kujiunga na Simba msimu ujao akitokea Zanaco ya nchini kwao kuchukua nafasi ya Bernard Morrison.

Moses Phiri Simba SCTaarifa zaidi zimeeleza kuwa Phiri atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Simba kwa wale wapya ambao watajiunga na timu hiyo msimu ujao wa 2022/2023 kutokana na kila kitu kikamilika na kinachosubiriwa ni tiketi tu ya ndege.

Klabu ya Young Africans kushirikiana na GSM wamepanga kufanya usajili wa gharama kubwa ambao utaifanya kutimiza malengo ya kuchukua Ubingwa kwa mara nyingine lakini pia kutikisa katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa msimu ujao wa 2022/2023.

Ili kupisha ujio wa wachezaji hao wapya, Klabu ya Young Africans imepanga kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji na wengine kuwapa mkono wa kwaheri moja kwa moja..

Taarifa ambazo Nijuze Habari imezipata ni kuwa Young Africans ina mpango wa kusajili wachezaji wanne ambao ni; winga mmoja, mshambuliaji mmoja wa kati, kiungo mshambuliaji, kiungo mkabaji pamoja na beki wa kushoto.

Aziz Ki Young Africans SCKatika orodha ya wachezaji wanaotajwa miongoni mwao ni nyota wa ASEC Mimosas, Aziz Ki ambaye anayewindwa pia na Zamalek ya Misri lakini upande wa winga, jina la mchezaji wao wa zamani aliyetemwa na Simba, Bernard Morrison limewekwa katika hesabu zao.

Wengine ambao wanatajwa kuwaniwa na Young Africans ni washambuliaji Victorien Adebayor na Moses Phiri ambaye pia anawaniwa na watani zao Simba SC pamoja na beki Mustafa Kiiza.

Victorien Adebayor Young Africans SCAidha wachezaji takribani sita watapewa mkono wa kwaheri kwa kuvunjiwa mikataba yao au kutoongezwa mipya baada ya ile ya awali kumalizika kutokana na viwango vyao kutoridhisha na kutoonekana kama wanaweza kuwa na mchango mkubwa.

Makipa Erick Johora na Ramadhan Kabwili watatupiwa virago moja kwa moja sambamba na Deus Kaseke, Chico Ushindi, Heritier Makambo na Paul Godfrey ‘Boxer’.

Heritier Makambo vs Deus Kaseke Yanga SCJohora, Kabwili, Makambo na Ushindi mikataba yao itavunjwa wakati Kaseke na Boxer hawataongezewa mikataba mipya.

Mshambuliaji wa Burkina Faso, Yacouba Sogne yeye ataongezwa mkataba, lakini atatolewa kwa mkopo ili apate timu itakayompa nafasi ya kutosha ya kucheza ili aweze kurudisha ufiti kama ilivyothibitishwa na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said.

Yacouba Sogne Yanga SCBaada ya kuwepo kwa tetesi kuwa Klabu ya Al Ahly ina mpango wa kumtoa kwa mkopo winga wake, Luís Miquissone, inaelezwa kuwa Uongozi wa Klabu ya Simba SC umemfuata mchezaji huyo kutaka kumrejesha Msimbazi.

Miquissone ambaye alikuwa mchezaji wa Simba kwa kipindi cha msimu mmoja na nusu kuanzia January 2020 hadi August 2021, tangu ajiunge na Al Ahly amekuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza chini ya Kocha Pitso Mosimane.

Luís Miquissone Al Ahly SCWinga huyo raia wa Msumbiji, anapata upinzani mkubwa kutoka uwepo wa Percy Tau raia wa Afrika Kusini ambaye ndiye mchezaji anayetegemewa eneo la winga.

Taarifa ambazo Nijuze Habari imezipata ni kuwa klabu ya Young Africans SC imefikia makubaliano na beki wa kushoto wa kimataifa wa Uganda, Mustafa Kizza kwa mkataba wa miaka 2

Mustafa Kizza Yanga SCKizza atajiunga na Wananchi kama mchezaji huru baada ya kuondoka Montréal inayoshiriki ligi Kuu ya (MLS) January 2022.

Tetesi zinadai kuwa Klabu ya Azam FC ina mpango wa kuwaacha baadhi ya wachezaji wakigeni ambao ni;

Never Tigere Azam FCMathias Kigonya
Nicolas Wadada
Yvan Mbala
Never Tigere
Idris Mbombo

Saido Ntibazonkiza Yanga SCKatika hatua nyingine umeelezewa kuwa Winga wa Klabu ya Young Africans Saido Ntibazonkiza amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Jangwani Jijini Dar es salaam.

Abdumajid Mangalo Biashara United FCKlabu ya Azam FC imetajwa kuwa kwenye mazungumzo ya Usajili na beki wa kati wa Biashara United Abdumajid Mangalo.

Mtenje Albano Coastal Union FCKlabu ya Diamond Trust Bank FC (DTB) imetajwa kuwa kwenye mazungumzo na kiungo mkabaji wa Coastal union FC ya Tanga Mtenje Albano.

Mpapi Nasibu Biashara United FCBaada ya kudumu kwa miaka minne (4) sasa, beki kisiki wa klabu ya Biashara United FC ya Mkoani mara, Mpapi Nasibu ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa Msimu huu wa 2022/2023 baada ya mkataba wake kufika kikomo.

Bakari Nondo Mwamnyeto Yanga SCBeki wa kati wa Young Africans SC, Bakari Nondo Mwamnyeto amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Jangwani Jijini Dar es salaam.

Mwamnyeto alijiunga na Young Africans July 2020 kutoka Coastal Union ya Tanga na amekuwa na misimu miwili mizuri ya awali hadi kupewa unahodha wa timu hiyo.

Kibwana Ally Shomari Yanga SCBeki chipukizi wa Klabu ya Young Africans, Kibwana Ally Shomari naye amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Klabu hiyo.

Shomari ambaye mkataba wake wa awali aliosaini 2020 akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro unamalizika mwezi ujao, sasa ataendelea kuwa mali ya wanachi hadi June 2024.

Zemanga Soze Simba SCImeelezwa kuwa Klabu Simba imepiga hodi kunako TP Mazembe kumfuata mshambuliaji Zemanga Soze mwenye umri wa miaka 22 kwaajili ya kufanya naye mazungumzo ya kumsajili misimu wa 2022/2023, Ili kuchukua nafasi ya Chris Mugalu anayemaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu.

Yunus Sentamu Simba SCAidha wapo baadhi ya washambuliaji wanaotajwa kuwaniwa na Simba katika kukisuka kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao na kati yao ni Yunus Sentamu anayeichezea AS Vita ya DR Congo na timu ya taifa ya Uganda.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA TANO 2022

AJIRA za Sensa ya Watu na Makazi 2022, Tazama hapa jinsi ya kujaza fomu

MATOKEO Azam FC vs Simba SC, May 18,2022

KIKOSI Cha Tanzania Kufuzu AFCON 2023

MATOKEO Yanga SC vs Mbeya Kwanza FC, May 20,2022

MAGAZETI ya Tanzania Jumatatu May 23,2022

MAGAZETI ya Tanzania Jumanne May 24,2022

MSIMAMO na Vinara wa NBC Premier League May 23,2022

MATOKEO Biashara United FC vs Yanga SC May 23,2022

MAGAZETI ya Tanzania Jumatano May 25,2022

VIINGILIO Nusu Fainali Yanga SC vs Simba SC (FA) May 28,2022

MAGAZETI ya Tanzania Alhamisi May 26,2022

SAFARI ya Yanga SC na Simba SC kwenye (ASFC) msimu huu wa 2021/2022

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.