Nijuze Habari

TETESI za Usajili Tanzania Bara June 12,2022

Filed in Usajili by on 12/06/2022 0 Comments

Moses Phiri Simba SCKlabu ya Simba imeendelea kukijenga kikosi chake kwaajili ya msimu ujao wa 2022/2023, taarifa rasmi zinadai kuwa wekundu hao wa msimbazi tayari wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Klabu ya Zanaco na Zambia, Moses Phiri mwenye umri wa miaka 29.

Nijuze Habari Application

TETESI za Usajili Tanzania Bara June 12,2022

Moses Phiri Simba SCKlabu ya Simba imeendelea kukijenga kikosi chake kwaajili ya msimu ujao wa 2022/2023, taarifa rasmi zinadai kuwa wekundu hao wa msimbazi tayari wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Klabu ya Zanaco na Zambia, Moses Phiri mwenye umri wa miaka 29.

Lazarous Kambole Yanga SCKlabu Young Africans SC imeripotiwa kushinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Keizer Chiefs ya Afrika Kusini, Lazarous Kambole mwenye umri wa miaka 28 kwa mkataba wa miezi 6 wenye chaguo la nyongeza ya miaka miwili.

Young Africans ikifanikiwa kukamilisha usajili huo itakuwa imeipiku klabu ya Zesco United katika mbio za mshambuliaji huyo raia wa Zambia ambaye amefunga magoli mawili tu katika mechi 46 kwa kipindi cha miaka miwili alichokuwa klabuni hapo.

Stephane Aziz Ki Yanga SCHabari njema ziwafikie wanachama na mashabiki wa Klabu ya Young Africans kuwa sasa ni uhakika msimu ujao eneo la ushambuliaji la timu hiyo atakuwapo staa kutoka Burkina Faso, Stephane Aziz Ki baada ya kumalizana na klabu hiyo na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Usajili wa Aziz Ki mwenye umri wa miaka 26 kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast kutua kwa Mabingwa wapya wa NBC Premier League 2021/2022 Young Africans umefikia kati ya asilimia 80-90.

Nassor Kapama Simba SCKlabu ya Simba SC imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mzawa Nassor Kapama anayekipiga kunako Klabu Kagera Sugar ya Kagera, mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.

Licha ya kucheza kama beki wa kati pale Kagera Sugar FC, Kapama pia anamudu nafasi ya kiungo inayochezwa na Jonas Mkude, Thadeo Lwanga, Sadio Kanoute na wengine pale Msimbazi, huku akicheza kama mshambuliaji na ana mabao mawili na assist 3 za mabao mpaka sasa Ligi inapoelekea mwishoni.

Clatous Chotta Chama Simba SCKatika hatua nyingine, viungo wa Klabu ya Simba SC, Clatous Chama na Rally Bwalya wameungana na timu hiyo katika mazoezi yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena.

Rally Bwalya Simba SCChama alirejea akitokea kwao Zambia alipokuwa kwaajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha mkewe, Mercy Mukuka kilichotokea May 29, 2021, Rally Bwalya yeye amerejea kutoka kwenye majukumu ya timu yake ya Zambia iliyokuwa ikijiandaa na michezo ya kufuzu AFCON 2023 nchini Ivory Coast.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Young Africans, Senzo Mazingisa amesema kuwa klabu hiyo imepokea ofa mbili kwaajili nyota wao raia wa DR Congo Fiston Kalala Mayele.

Fiston Kalala Mayele Yanga SCSenzo amesema kuwa Kaizer Chief na Berkane zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya nyota huyo lakini klabu hiyo haina mpango wa kuumuza Kinara huyo wa mabao ndani ya Klabu hiyo na Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 14 sawa na Mshambuliaji mzawa George Mpole Mwaigomole kutoka Geita Gold FC ya Geita.

Nathaniel Chilambo Azam FCKlabu ya Azam FC imekamilisha uhamisho wa Mlinzi wa Kulia wa Klabu ya Ruvu Shooting Nathaniel Chilambo pamoja Abdulimajid Mangalo kutoka Biashara United FC kwa mkataba wa Miaka miwili.

Saido Ntibazonkiza Simba SCKlabu ya Simba SC imetajwa kuwa katika mazungumzo na kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza mwenye umri wa miaka 35 raia wa Burundi baada ya kuachwa na watazi zao Young Africans SC.

Klabu ya Simba SC pia imetajwa kuwa kwenye mazungumzo na Mshambuliaji wa Geita Gold FC ya mkoani Geita George Mpole mwenye umri wa miaka 29.

George Mpole Simba SCMpole mwenye mabao 14 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) anatajwa kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Geita Gold FC.

Cesar Manzoki Simba SCSimba pia inawinda saini ya Mshambuliaji wa Vipers ya Unganda, Cesar Manzoki mwenye umri wa miaka 25, ambaye alijiunga na Vipers akitokea AS Vita Club ya DR Congo mwaka 2020.

Aidha Klabu ya Simba SC, jana Jumamosi June 11,2022 uliwataka wapenzi na wanachama wake kupuuza barua inayoenea kwenye mitandao ya kijamii ikihusisha klabu hiyo kutoa ofa kwa kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas Stephen Aziz Ki.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.