UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

Filed in Makala by on 25/03/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake, Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa huu wa Marburg uligundulika kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani mwaka 1967 katika Mji wa Marburg na ndio asili ya jina la ugonjwa huu.

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake,Marburg virus death rate,Marburg virus news,Marburg virus transmissionMarburg virus outbreak 2023,Marburg virus symptoms,Marburg virus year,Marburg virus outbreak,What does Marburg virus do,Where is Marburg virus found,Marburg virus outbreak

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

Ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine hususani kwa njia ya kugusa majimaji ambayo yanaweza kuwa mate, mkojo, damu, machozi au kinyesi yatokayo kwenye maiti au mgonjwa mwenye dalili.

Maambukizi pia yanaweza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu iwapo mtu atakula au kugusa mizoga au wanyama walioambukizwa, ugonjwa huo hauna tiba mahususi isipokuwa hutibiwa kulingana na dalili.

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

Kwa Tanzania ugonjwa huo umegundulika katika kata za Maruku na Kanyangereko zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini Mkoani Kagera ambapo hadi sasa jumla ya kesi nane zimeripotiwa, kati yao watano pekee ndio wamefariki.

Serikali yakiri uwepo wa Ugonjwa usiojulikana Kagera

Miongoni mwa mataifa ya Afrika ambayo yamewahi kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kenya, Afrika Kusini, Uganda, Zimbabwe na Angola.

Dalili Za Ugonjwa Wa Marburg

Dalili za awali ni pamoja na homa, kuumwa na kichwa na Kuumwa na misuli, dalili za baadaye ni kikohozi, maumivu ya viungo, kuhara na kutapika, na mara nyingi hata upungufu wa damu katika mwili.

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa Baadhi ya watu hutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili na kufa siku nane hadi tisa baada ya kuugua kwa sababu ya kupoteza damu nyingi na mshtuko.

Kwa wastani, virusi huua nusu ya walioambukizwa, WHO inasema, lakini aina hatari zaidi imeua hadi 88%.

MARBURG NI NINI?

Marburg virusMlipuko huo ulitokana na tumbili wa Kiafrika walioagizwa kutoka Uganda. Lakini virusi hivyo vimehusishwa na wanyama wengine tangu wakati huo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt, Ujerumani na Belgrade huko Serbia.

Na miongoni mwa wanadamu, huenezwa zaidi na watu ambao wamekaa kwa muda mrefu katika mapango na migodi yenye popo.

Inaeneaje?

Popo wa matunda aina ya rousette wa Misri mara nyingi huwa na virusi. Nyani wa kijani kibichi na nguruwe wanaweza pia kubeba.

Miongoni mwa wanadamu, huenea kupitia maji ya mwili na malazi yaliyochafuliwa nao, na hata watu wakipona, damu au shahawa zao, kwa mfano, zinaweza kuwaambukiza wengine kwa miezi mingi baadaye.

Matibabu

Hakuna chanjo maalumu wala matibabu ya virusi hivi.

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na dalili zake

Namna ya kujikinga na Ugonjwa wa Marburg

• Epuka kula au kushika nyama ya porini katika maeneo yenye mlipuko.

• Epuka kuwa karibu na nguruwe katika maeneo yenye mlipuko, WHO inasema.

• Wanaume ambao wamekuwa na virusi wanapaswa kutumia kondomu kwa mwaka mmoja baada ya kupata dalili au hadi mbegu zao zitakapothibitishwa mara mbili kuwa hazina virusi.

• Kwa wale wanaozika watu ambao wamekufa kutokana na virusi wanapaswa kuepuka kugusa mwili.

Milipuko mikubwa kuwahi

2017, Uganda: visa – 3, Vifo – 3

2012, Uganda: visa – 15, Vifo – 4

2005, Angola: visa 374, Vifo – 329

1998-2000, DR Congo: visa – 154, Vifo – 128

1967, Ujerumani: visa 29, Vifo – 7. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN).

UNAWEZA PIA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *