UGONJWA wa Marburg wathibitiwa Kagera Karantini wafikia 205

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


UGONJWA wa Marburg wathibitiwa Kagera Karantini wafikia 205

UGONJWA wa Marburg wathibitiwa Kagera, Karantini wafikia 205
Idadi ya washukiwa wa Ugonjwa Wa Marburg Mkoani Kagera imefikia watu 205 Kutoka 193 kama ilivyokuwa imeelezwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumain Nagu Machi 23, (2023).
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu March 25, 2023 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Manispaa ya Bukoba na kusema mpaka sasa hakuna visa vipya vya wagonjwa wala kifo kilichotokea.
Waziri Ummy amesema kuwa, wataalamu wa afya wanaendelea kufuatilia watu wote waliochangamana na wagonjwa wa Marburg na kuwaweka karantini kwa kipindi cha siku 21 ili kubaini kama wana dalili za ugonjwa huo ambao mtu anaambukiza baada ya kuonyesha dalili.
Amesema kutokana na kiini cha mgonjwa kutokea Kisiwa cha Gozba wametuma timu ya wataalamu kutoka Wilaya ya Muleba ambao watafanya ufuatiliaji kubaini wale wote waliochangamana na mgonjwa huyo ambaye baada ya kutoka kisiwani alikwenda kwenye familia yake Maruku.
Ummy Mwalimu amesema kuwa, “bado tuna visa nane ikiwa ni vifo vitano na watu watatu bado wanaendelea na mabibabu, lakini washukiwa waliochangamana na wagonjwa wameongezeka na kufikia 205, ambao ni wanafamilia na wataalamu wetu wa afya waliohudumia wagonjwa hao, hii ni dhahili kuwa ugonjwa huu haujatoka nje ya familia ambazo zimeathiliwa na ugonjwa huo.”
Aidha, amesema kuwa watu hao waliotengwa sio wagonjwa na hawana dalili zozote ila wamezuiliwa kwa muda ili kuwalinda wenyewe endapo watapata dalili pamoja na kuilinda jamii huku akisisitiza kuwa mtu kama hana dalili za ugonjwa huo hawezi kumuambukiza mtu mgonjwa mwingine.
Hata hivyo, ameongeza kuwa timu ya wataalamu wabobezi wa kupambana na ugonjwa huo wameishawasili mkoani Kagera ili kusaidizana na wataalamu wengine wa afya walioko mkoani humo huku akiwataka wananchi mkoani Kagera kuendelea kuchukua taadhari za kujikinga na ugonjwa huo kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka pamoja na kutumia vitakasa mikono.
Waziri Ummy amebainisha kuwa, Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa afya wanaendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kuanza kupima joto la wasafiri wote wanaoingia na kutoka nje ya Mkoa wa Kagera, huku akiwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kuwaingizia kipato.
Amesema wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao 1322 wamepata ajira ya muda wa miezi mitatu mkoani Kagera kwaajili ya kusaidia Kutoa elimu ngazi ya jamii katika kumsaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Marburg.
‘Katika juhudi za serikali za kupambana na ugonjwa wa Marburg tutayatumia makundi matatu ambayo ni wahudumu wa afya ngazi ya jamii, viongozi wa dini na waganga wa kienyeji. Tumeajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao 1,322 ambao watakuwa katika mkoa mzima lakini kwa sasa tumeanza na halmashauri mbili Bukoba Vijijini na Bukoba manispaa na wahudumu hao tutawaweka kila kitongoji wawili, mtaa watatu na kila kijiji mmoja,” amesema Waziri Ummy.
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani -WHO, Zabron Yoti amesema juhudi zinazofanywa kudhibiti ugonjwa huo kwasasa ikiwa ni siku tisa tu tangu utangazwe na ukiwa na visa vichache, ni kwaajili ya kuzuia mapema usisambae maeneo mengine.
Aidha kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Issesanda Kaniki amesema kuwa, kwa kushirikiana na Manispaa ya Bukoba pamoja na wadau wengine watafanya mwendelezo wa kuweka vifaa vya kunawia mikono katika maeneo ya kituo kikuu cha mabasi pamoja na Soko Kuu.
Pia katika Barabara ya Magari yaendayo Geita, Mwanza Kahama, Dar es Salaam na mikoa mingine kitawekwa kituo maeneo ya Kemondo ili abiria wote wapimwe joto na Barabara ya kwenda Karagwe, Mtukula pia eneo la Kyaka Misenyi kitawekwa kituo cha kupima abiria wote wanaotokea Barabara hiyo.
Waziri Ummy atatembelea Kata ya Maruku na Kayangereko ambapo walipatikana wagonjwa wa Marburg na atatembelea eneo ambalo watu 205 wamewekwa karantini pamoja na kituo cha matibabu ya wagonjwa wa Marburg.
Hadi sasa serikali kupitia wataalamu wa afya wameendelea kutoa Elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo na wagonjwa watatu wanaendelea na matibabu.
Waziri Ummy ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Kagera na wataalamu wote wa afya kwa kuwa mstari wa mbele kukabiliana na ugonjwa huo kwa jitihada zote zilizochukuliwa kwa kushirikiana kikamilifu na Wizara ya Afya katika kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.
UNAWEZA PIA KUSOMA👇
- MSIMAMO Kundi D CAF Confederation Cup 2022-2023
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: UGONJWA wa Marburg wathibitiwa Kagera Karantini wafikia 205