Nijuze Habari

UGONJWA wa nyani tishio jipya la afya Duniani

Filed in Habari by on 25/07/2022 0 Comments

UGONJWA wa nyani tishio jipya la afya DunianiSHIRIKA la Umoja wa Mataifa la afya Ulimwenguni, (WHO), limetangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa ndui ya nyani au monkeypox Duniani kuwa ni tishio kwa afya ya umma.

Nijuze Habari Application

UGONJWA wa nyani tishio jipya la afya Duniani

UGONJWA wa nyani tishio jipya la afya DunianiSHIRIKA la Umoja wa Mataifa la afya Ulimwenguni, (WHO), limetangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa ndui ya nyani au monkeypox Duniani kuwa ni tishio kwa afya ya umma.

Tangazo hilo, limetolewa July 23, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Geneva, Uswisi baada ya kikao cha pili cha Kamati ya Kimataifa ya dharura za kiafya ya WHO kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa ndui ya nyani au Monkeypox.UGONJWA wa nyani tishio jipya la afya Duniani

Dkt. Tedros alisema kuwa ingawa wajumbe wa kamati hawakufikia muafaka kuhusu ndui ya nyani kama ni tishio au la kwa mujibu wa vigezo vya kutoa tamko hilo, ametangaza kuwa mlipuko ni tishio na umeenea zaidi Ulaya.

Kwa mujibu wa Dkt. Tedros, mlipuko umeendelea kukua na hadi sasa kuna waonjwa zaidi ya 16,000 kutoka nchi 45 Duniani na vifo vya watu watano vimeripotiwa.UGONJWA wa nyani tishio jipya la afya Duniani

Amesema, kilichobainika ni kwamba ugonjwa huo unasambaa zaidi miongoni mwa wanaume mashoga na wenye wapenzi zaidi ya mmoja na hivyo ni vyema kuchukua hatua kujikinga na iwapo hatua zitachukuliwa, ugonjwa huo unaweza kudhibitiwa na mlipuko kudhibitiwa pia.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.