Nijuze Habari

UMRI wa miaka 18 + kuanza kulipa Kodi

Filed in Habari by on 16/06/2022 0 Comments

UMRI wa miaka 18 + kuanza kulipa KodiWaziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuanza kulipa kodi.

Nijuze Habari Application

UMRI wa miaka 18 + kuanza kulipa Kodi

UMRI wa miaka 18 + kuanza kulipa KodiWaziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuanza kulipa kodi.

Dk Mwigulu amebainisha hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.

Waziri huyo amesema ili kufikia azma hiyo wataanza kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania  kuanzia umri wa kuanzia miaka 18 kwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unaomtaka kila mwananchi mwenye umri huo wa au zaidi kujisajili.

“Napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi,”amesema

Waziri huyo amefafanua kuwa kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.