Nijuze Habari

UTARATIBU wa kupata cheti cha kuzaliwa Tanzania na walio nje ya nchi

Filed in Habari by on 28/05/2022 0 Comments

RITA Jinsi Ya Kupata Cheti Cha Kuzaliwa | How To Get Birth Certificate Tanzania

Nijuze Habari Application

UTARATIBU wa kupata cheti cha kuzaliwa Tanzania na walio nje ya nchi

RITA Jinsi Ya Kupata Cheti Cha Kuzaliwa | How To Get Birth Certificate Tanzania

Registration of births is governed by the Births and Deaths Registration Act, (CAP 108, R.E 2002)

According to the law a birth is require to be registered within 90 days of the occurrence and a Death within 30days, and that  event Must be occured within the borders of mainland Tanzania.However, the law allows for late registration. The duty to register a birth lies on the following:

UTARATIBU wa kupata cheti cha kuzaliwa Tanzania | How To Get Birth Certificate Tanzania

USAJILI WA VIZAZI UNASIMAMIWA NA sheria ya uandikishaji vizazi na vifo,(sura 108 toleo la 2002)

Kulingana na sheria kizazi inatakiwa kuandikishwa ndani ya siku 90 tangu kutokea kwake na kifo ndani ya siku30, na Tukio hilo Lazima liwe limetokea ndani ya mipaka ya Tanzania Bara.Pamoja na takwa hili sheria inaruhusu usajili kufanyika nje ya muda huu.Wajibu wa kusajili kizazi ni kama ufuatao:

NB: Baba au Mama,na kama Baba na Mama hawapo,mmiliki wa nyumba ambaye ana taarifa za kizazi kutokea,mtu yoyote ambaye amekuwapo wakati kizazi kikitokea au mtu yoyote ambaye mtoto aliyezaliwa yuko katika himaya yake.

UTARATIBU WA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA

1: Usajili wa kizazi ndani ya siku 90

 • Kama kizazi kimetokea hospitalini,kituo cha afya au zahanati hakikisha unapatiwa Tangazo la kizazi kabla ya kuondoka.
 • Endapo kizazi kitakuwa kimetokea nyumbani,toa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa kijiji au Msajili wa vizazi au vifo wa wilaya ili ipatiwe tanzazo la kizazi.taarifa hii itolewe ndani ya siku 90.
 • Wasilisha tangazo la kizazi kwa msajili wa vizazi na vifo wa wilaya kilipotokea kizazi
 • Lipa ada ya cheti inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 3500/=).

2: Usajili nje ya siku 90 lakini chini ya miaka 10.

 • Jaza na wasilisha Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3  (ijazwe na mzazi au mlezi)
 • Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
 • Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono maelezo yako kwenye fomu.nyaraka hizi ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
 • Lipia ada inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 4000/=) kwa wilayani na shilingi elfu 14,000/= kwa makao makuu

3: Kuandikisha kizazi kilichochelewa kuandikishwa zaidi ya miaka 10

 • Jaza na wasilisha  Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3 (ijazwe na mzazi au mlezi).
 • Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
 • Ambatanisha nyaraka ,kadi ya kliniki ya mtoto,cheti cha ubatizo kamakipo,barua kutoka mamlaka ya serikali zinazohusika kama vile ofisi ya mtendaji kata au kijiji),cheti cha kumaliza elimu ya msingi, cheti cha kumaliza elimu ya sekondari  kuthibitisha tarehe ya kuzaliwa,mahali pa kuzaliwa na uraia wa wazazi.
 • Kwa watu walio zaliwa zamani sana unapaswa kuwa na viambatanisho viwili ambapo utatakiwa kuwa na kadi ya utaifa pamoja naya kura au bima ya afya, kama mwombaji anataka kutumia kadi ya leseni ya gari lazima iambatane pamoja na kadi ya utaifa au ya kura.
 • Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tshs 10,000/=) kwa wilayani na shilingi 20,000/= kwa makao makuu.

4: Kupata nakala ya cheti baada ya kupoteza.

 • Wasilisha ombi lako ukionesha namba ya ingizo jina la mwenye cheti,mahali pa kuzaliwa na tarehe ya kusajiliwa.
 • Jaza taarifa zako katika Fomu ya kutafutia kumbukumbu (search form)
 • Lipa ada inayotozwa (ada ya sasa ni Tsh.3500/= ikiwa Tshs.1500/= ada ya upekuzi na Tsh 2000/= ada ya makala ya cheti.

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa

 • Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa
 • Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako – barua inayotetea ombi lako na kiambatanisho(cheti cha ubatizo,kadi ya clinic au vyeti vya shule na vielelezo vingine msajili atakavyohitaji kwaajili ya kujiridhisha, vielelezo vya wazazi kama vile cheti cha kuzaliwa, vyeti vya vifo au vitambulisho vyao  ikiwa jina la mmoja wa wazazi limekoseewa)
 • Rejesha cheti kinachotakiwa kusahihishwa.
 • Ada baada ya ombi lako kukubaliwa (ada ya sasa ni Tsh6500/=(ikiwa ni:-3000/= ada ya kusahihisha , 1500/= ada ya upekuzi na 2000/= ada ya cheti)

TANBIHI:

 1. Kubadili au kuongeza jina.
  Sheria inaruhusu kubadili au kuongeza jina ndani ya miaka miwili tangu tarehe ya kusajiliwa.Baada ya muda huu kupita daftari la kizazi haliwezi kurekebishwa kwa badiliko la jina,mhusika atatakiwa kufuata utaratibu mwingine chini ya sheria ya kubadili jina kwa ajili ya (Deed polls).
 2. Taratibu mpya za kupata vyeti vya kuzaliwa kwa walio nje ya nchi.soma zaidi

>> MASWALI MBALI MBALI YANAULIZWA KUHUSU VIZAZI

Utaratibu wa Kupata Cheti cha Kuzaliwa, kwa Watu Walio nje ya Nchi.

Hatua ya Kwanza:
 • Tuma barua pepe ya maombi kupitia info@rita.go.tz
 • Ambatanisha na kimojawapo kati ya viambatanishi vifuatavyo (Clinic card, Cheti cha ubatizo, School leaving certificates [Shule ya msingi, Sekondari]), kwa uhakika wa tarehe ya kuzaliwa mtoto, sehemu ya uzaliwa na uraia wa wazazi.
 • Pakuwa fomu B3 (kwa Usajili wa mtoto zaidi ya siku 90, lakini chini ya miaka 10), au fomu B3 (kwa Usajili wa mtoto zaidi ya miaka 10). Jaza na zitume kwa barua pepe info@rita.go.tz
  Fomu za kupakuwa zinapatikana hapa

  Hatua ya Pili:

 • Utapokea barua pepe kutoka RITA, iliyoambatanishwa na fomu ya Afidavit, kutoka kwa Msajili Mkuu.
 • Printi na jaza fomu ya Afidavit, kisha iambatanishe na picha 3 za passport size.
 • Scan fomu ya Afidavit, itume kwa barua pepe kuelekea info@rita.go.tz

  Hatua ya Tatu:

 • Utapokea barua pepe kutoka RITA, ikikupa ruhusa ya kulipia.
 • Malipo ya kusafirisha cheti yatategemea huduma utakayoamua kutumia (DHL, EMS n.k)

  Malipo:

 • Cheti cha mtoto chini ya miaka 10 – $14.
 • Cheti cha mtoto zaidi ya miaka 10 – $20.
 • ku-clear cheque – $20.

  Tanbihi:

 • Utatakiwa ufanye uchunguzi ili kufahamu Malipo ya kusafirisha Cheti ni bei gani, halafu utume fedha (ya kulipia cheti), pamoja na fedha ya kukombolea mzigo(fedha).
 • Tunasisitiza malipo kwa fedha taslimu.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

Fahamu Jinsi ya kupata namba ya NIDA (NIN)

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA TANO 2022

AJIRA za Sensa ya Watu na Makazi 2022, Tazama hapa jinsi ya kujaza fomu

MATOKEO Azam FC vs Simba SC, May 18,2022

KIKOSI Cha Tanzania Kufuzu AFCON 2023

MATOKEO Yanga SC vs Mbeya Kwanza FC, May 20,2022

MSIMAMO na Vinara wa NBC Premier League May 23,2022

MATOKEO Biashara United FC vs Yanga SC May 23,2022

MAGAZETI ya Tanzania Jumatano May 25,2022

VIINGILIO Nusu Fainali Yanga SC vs Simba SC (FA) May 28,2022

MAGAZETI ya Tanzania Alhamisi May 26,2022

SAFARI ya Yanga SC na Simba SC kwenye (ASFC) msimu huu wa 2021/2022

TETESI za Usajili Tanzania Bara 2022/2023

MAGAZETI ya Tanzania Ijumaa May 27,2022

MAGAZETI ya Tanzania Jumamosi May 28,2022

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.