Nijuze Habari

VETA yabuni Mashine ya kukausha nguo za ndani

Filed in Habari by on 05/08/2022 0 Comments

VETA yabuni Mashine ya kukausha nguo za ndaniMAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia Chuo cha Ufundi Stadi cha Dar es Salaam kimebuni mashine ya kukausha nguo za ndani kinachoitwa (Dhydrator) Mashine lengo likiwa ni kutokomeza magonjwa ya fangasi na urinary tract infection, U.T.I.

Nijuze Habari Application

VETA yabuni Mashine ya kukausha nguo za ndani

VETA yabuni Mashine ya kukausha nguo za ndaniMAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia Chuo cha Ufundi Stadi cha Dar es Salaam kimebuni mashine ya kukausha nguo za ndani kinachoitwa (Dhydrator) Mashine lengo likiwa ni kutokomeza magonjwa ya fangasi na urinary tract infection, U.T.I.

Aidha Watanzania wametakiwa kukubali teknolojia ambazo zinabuniwa na wazawa ili kuwapa hamasha ya kuongeza juhudi katika bunifu zao ikiwa ni pamoja na kununua bidhaa wanazozibuni.

Akizungumza leo jijini Mbeya katika maonyesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu (Nanenane) yanayoendelea viwanjani John Mwakangale, Mbunifu wa mashine hiyo, Emmanuel Bukuku, amesema kuwa Watanzania wanaamini bidhaa zinazotoka China kuliko kuuamini zinazobuniwa nchini.

Bukuku amesema kuwa baada ya kuona changamoto ya uanikaji wa nguo za ndani alikaa chini na kubuni mashine ambayo itaondoa changamoto hiyo ya kukausha nguo hizo kwa muda mfupi na mashine hiyo inatumia umeme kidogo.

Amesema kuwa nguo za ndani mara nyingi zikifuliwa huwa zinaanikwa ndani hali inayowasababishia watumiaji kupata magonjwa kutokana na kukuza wadudu ambao wanasababisha magonjwa kama fangasi.

Amesema kilichomsababishia kubuni mashine hiyo ni baada ya kuona jamii ina changamoto ya kupata magonjwa kama vile fangasi ya ngozi na U.T.I kwa watu wazima na watoto hivyo kifaa hicho kitasaidia kupunguza magonjwa hayo au kuyatokomeza kabisa.

“Kwa upande wa afya hii ni teknolojia nzuri na jamii bado haijajua hii mashine kwa ubunifu huu tunaweza kuwakomboa watoto wengi wanaokumbana na magonjwa ya U.T.I na fangasi, pamoja na wanawake hii inaweza kuwa mkombozi kwao,”ameongeza.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.