VIINGILIO Simba vs ASEC Mimosas 25 November 2023
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
VIINGILIO Simba vs ASEC Mimosas 25 November 2023
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba SC, Ahmed Ally ameanza kampeni ya hamasa kuelekea mchezo wa kwanza Makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.
Klabu ya Simba inatarajiwa kuanzia nyumbani November 25,2023, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 10 jioni.
Kuelekea mchezo huo Simba italazimika kushinda mechi zote za nyumbani ili kuwa na nafasi nzuri ya kutinga robo Fainali ya michuano hiyo.
Amed amesema kuwa ASES Mimosas watawasili November 23, 2023 wakiwa na msafara wa watu 31, huku waamuzi wa mchezo wakitoka nchini Misri.
Viingilio vilivyopangwa ni kama inavyoonekana hapa chini!
“Viingilio vya mchezo huu ni;
Mzunguko – Tsh. 5,000.
VIP C – Tsh. 10,000.
VIP B – Tsh. 20,000.
VIP A – Tsh. 30,000
Platinum – Tsh. 150,000.”
Matokeo ya ushindi kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas yatakuwa na maana kubwa kwa kikosi cha Simba. Kwani yatarudisha morali ya timu na alama tatu muhimu nyumbani.
Aidha Simba ina mashabiki bora barani Afrika, hili limethibitishwa na CAF wenyewe baada ya michuano ya AFL kushinda tuzo ya Mashabiki Bora.
Silaha ya mashabiki ni muhimu sana katika mechi hizi zenye mfumo wa mtoano.
VIINGILIO Simba vs ASEC Mimosas 25 November 2023
“Kikosi kipo mazoezini kuanzia siku ya Jumatatu. Mazoezi yanawahusu wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za taifa. Ambao wapo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao wakitoka huko. Kikosi bado kipo chini ya Kocha Seleman Matola na Dani Cadena. Uongozi unaendelea na jitihada za kutafuta kocha mpya, mchakato utakamilika muda si mrefu.”
“Tupo katikati ya mashindano lazima tutafute kocha ambaye yupo active, atakuwa tayari kuanza majukumu ili akifika kazi ianze.”
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.
“Kuhusu majeruhi Kibu tayari amerudi, Kanoute anaendelea vizuri, Isra Mwenda tayari amerudi mazoezini na Kramo bado anaendelea kuuguza jeraha. Akipona atarudi kutumikia klabu.”
“Wageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba. Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi.”
“Tusahau yaliyopita na tuangalie mbele. Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa tukipoteza na tukiwa nyumbani hatutakuwa kwenye sehemu nzuri ya kwenda hatua ya mbele. Twendeni tukawape moyo wachezaji wetu kwamba tunaanguka pamoja na kusimama pamoja.”- amesema Ahmed Ally.
“Siku hiyo tukawaonyeshe sisi ni mashabiki bora kwa kuja wengi uwanjani. Lakini pia tuna wajibu wa kwenda kuipigani Simba yetu. Pamoja na yote uliyonayo moyoni lakini wewe ni shabiki wa Simba, ukisusa maana yake unainunia Simba yako.”
“Wachezaji sisi tuna imani nao, tarehe 25 wakaendeleze makubwa. Waamke sasa wakaipiganie Simba. Wanayo kazi kubwa ya kutufutia hizi kejeli kwa wao kufanya vizuri. Tukipata matokeo mazuri watapunguza machungu makubwa tunayopita hivi sasa.”
“Ni muhimu wajue pale hawachezi tu kwa ajili yao bali kwa ajili ya Simba. Sisi tutaenda kutimiza wajibu wa kushangilia, na wao watupe furaha ili turejeshe hali yetu ya kutamba. Tunawambia hivyo kwa niaba ya mgeni rasmi, mashabiki wa Simba.”
“Tutakuwa na hamasa kama kawaida, na tutaanza mapema kuanzia Jumatatu tukiwa na matukio mbalimbali ya kuwahamasisha mashabiki kuja uwanjani. Ratiba tutatoa Jumapili ya mtaa kwa mtaa. Tunataka kuujaza Uwanja wa Mkapa, tuwaonyeshe kwamba hii ni Simba.”
“Tutakuwa na jezi maalumu ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kama mnavyojua mdhamini rasmi huwa hatumiki kwenye jezi ya mashindano hayo na kwa miaka ya nyuma tulikuwa tunatumia Visit Tanzania. Kuanzia Jumatatu tutatoa taarifa itakavyokuwa msimu huu.”
“Nimepewa baraka na viongozi wa klabu kutembelea matawi ya Simba nikianza na jana katika Tawi la Simba Soko la Samaki Msasani. Tunafanya hivi kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Wanasimba. Kupokea maoni yao na kuwaalika kuja uwanjani.”- Ahmed Ally.
“Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL 2023 haitakaa kwenye ofisi za Simba bali itakuwa inatembea kwenye matawi mbalimbali. Lakini pia tutakuwa na mfano ya tuzo kama hii ambayo tutaipeleka sehemu mbalimbali ili wabaki na kumbukumbu.”
“Kuhusu mabango tumeyaona na tuna kitengo cha sheria, wanaangalia kuona kama inafaa kuchukua hatua au kuacha lakini hili tumesababisha sisi. Wakati ujao wachezaji wafanye kila linalowezekana hiyo kadhia isitokee tena. Mwiba unatokea ulipoingilia.”
“Tiketi tunaanza kuuza leo, nunueni tiketi twendeni uwanjani. Ni kweli tulikuwa hatuchezi mpira wetu wa kuvutia lakini tunakwenda kubadilisha benchi la ufundi, tunategemea Simba itakayokuja kuwa na mabadiliko.”
“Safari hii tunakwenda kuwashangaza watu, tutaujaza uwanja wa Mkapa. Niwambie Wanasimba kama una hasira uje nazo furaha utaikuta uwanjani.”
“Kauli mbiu yetu ya mchezo dhidi ya ASEC Mimosas ni Twendeni Kinyama, Mashabiki Bomba.”- Ahmed Ally.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Tags: Simba SC vs ASEC 25 November 2023, Simba vs ASEC, Viingilio Simba ASEC CAF Champions League, viingilio Simba SC vs ASEC, Viingilio Simba SC vs ASEC Mimosas, VIINGILIO Simba vs ASEC Mimosas 25 November 2023, VIINGILIO Simba vs ASEC Mimosas 25 November 2023 | CAF Champions League, Viingilio Simba vs ASEC Mimosas Ligi ya Mabingwa Afrika