VIINGILIO Simba vs Horoya 18 March 2023

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


VIINGILIO Simba vs Horoya 18 March 2023
VIINGILIO Simba vs Horoya 18 March 2023,Viingilio Simba SC vs Horoya AC, viingilio Simba SC vs Horoya, Simba vs Horoya Athletic Club, Viingilio Simba Horoya CAF Champions League, Viingilio Simba vs Horoya AC Ligi ya Mabingwa Afrika,Simba SC vs Horoya AC Saturday 18 March 2023

VIINGILIO Simba vs Horoya 18 March 2023
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers ya Uganda , Klabu ya Simba inatatajiwa kucheza mchezo ujao wa Kundi (C) CAF Champions League dhidi ya Horoya AC ya Guinea.
Mchezo huo wa tano kwa timu zote unatarajiwa kuchezwa March 18, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam kuanzia saa 1:00 Usiku.
Kuelekea mchezo wa huo Simba imetaja Viingilio ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Tsh 3,000 kwa Mzunguuko.
Viingilio vilivyopangwa ni kama inavyoonekana hapa chini!
VIP A itakuwa Tsh 30,000
VIP B itakuwa Tsh 20,000
VIP C itakuwa Tsh 10,000
Mzunguko itakuwa Tsh 3,000
Platinum Sh. 150,000
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa tiketi za Executive nazo zitapatikana kwaajili ya vikundi au makampuni ambayo yatataka kuwanunulia wafanyakazi wake watapelekewa mpaka ofisini kwao.
Tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao, mashabiki wanasisitizwa kununua mapema ili kuepeuka usumbufu siku ya mchezo.
Simba inahitaji Ushindi wa lazima dhidi ya Horoya ili kujihakikishia nafasi ya pili kwenye Kundi hilo na moja kwa moja kutinga robo Fainali ya Michuano hiyo Mikubwa Afrika ngazi ya Vilabu.
Kwenye Msimamo wa Kundi C, Raja Club Athletic wanaongoza wakiwa na pointi 12, Simba wanafuatia wakiwa na pointi 6, Horoya AC ya Guinea ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4, huku Vipers SC wakiwa nafasi ya mwisho kwa pointi 1.
Vipers SC wao watawakaribisha Raja Casablanca kwenye Uwanja wa St Mary’s nchini Uganda March 18 pia na muda ule ule saa 1:00 Usiku.
Simba kwenye Mkutano na waandishi wa Habari leo Jumatatu Machi 13,2023 imesema kuwa, Kikosi kimeingia kambini kujiandaa na mchezo huo, ambapo Jana Jumapili wachezaji walipumzika lakini leo wameanza rasmi mazoezi.”
Kupitia Afisa Habari wa Klabu hiyo, Ahmed Ally, Simba imetoa taarifa za kupona kwa Mshambuliaji wake Kibu Denis na kuwa ataanza mazoezi pamoja na Wachezaji wenzake.
“Akili na nguvu zetu tunakwenda kuziweka Jumamosi ili tuweze kushinda na kufuzu Robo Fainali. Ni mechi yenye namna moja pekee tu kushinda. Mechi hii inatukumbusha mechi ya AS Vita, safari hii tupo na Horoya.”
“Kila Mwanasimba lazima atambue kwamba tutaingia Uwanja wa Mkapa kwenda kupambana kuingia Robo Fainali. Hatuko tayari kuishia hatua ya Makundi na wakati mechi ya kutupeleka robo tutachezea Uwanja wa Mkapa.”
“Waamuzi wote wa mchezo wanatokea nchini Misri. Waamuzi hawa wanne watawasili nchini alfajiri ya Machi 17, 2023.”
“Horoya wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe Machi 17, 2023 asubuhi.” amesema Afisa Habari wa Simba SC Ahmed Ally.
“Kauli mbiu yetu kuelekea mchezo huu ni TUNAITAKA ROBO FAINALI.”
“Hamasa safari hii ni tunataka kujaza Uwanja wa Mkapa, tutapita kila eneo kuhakikisha hakuna Mwanasimba anabaki nyumbani siku hiyo. Tayari tumeanza kuona matawi kutoka mikoani yakipanga kuja Dar.”
“Hamasa yetu tutazindulia Msumbuji, Chanika Msumbiji ambapo wenyeji wetu litakuwa tawi la Simba Chanika Msumbiji na tutaanza saa 5 asubuhi. Balaa letu litaanzia Pugu Mnadani. Nayaalika matawi yote pamoja na ndugu zetu wanahabari.”
“Hawa Horoya pamoja na ukubwa wao wote tukiwapigia kelele hakuna namna wanaweza kutoka. Hawajazoea kucheza kwenye mazingira magumu ambayo tutawaonyesha siku hiyo. Ukiweza jichanganye kabisa ukiwa unakuja uwanjani.”- ameongeza Ahmed Ally.
- SIMAMO Kundi D CAF Confederation Cup 2022-2023
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Simba SC vs Horoya AC Saturday 18 March 2023, Simba vs Horoya Athletic Club, Viingilio Simba Horoya CAF Champions League, viingilio Simba SC vs Horoya, Viingilio Simba SC vs Horoya AC, VIINGILIO Simba vs Horoya 18 March 2023, Viingilio Simba vs Horoya AC Ligi ya Mabingwa Afrika.