VIINGILIO Yanga vs US Monastir 19 March 2023

Filed in Michezo by on 15/03/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

VIINGILIO Yanga vs US Monastir 19 March 2023

VIINGILIO Yanga vs US Monastir 19 March 2023,Yanga vs Monastir leo, Viingilio Yanga vs US Monastir leo 19 March 2023,Viingilio Yanga vs Real Bamako CAF Confederation Cup,Viingilio Yanga SC vs US Monastir Kombe la Shirikisho Afrika leo,Yanga vs US Monastir Leo,Yanga dhidi ya Monastir leo tarehe 19.3.2023,Yanga vs US Monastir.

VIINGILIO Yanga vs US Monastir 19 March 2023,Yanga vs Monastir leo, Viingilio Yanga vs US Monastir leo 19 March 2023,Viingilio Yanga vs Real Bamako CAF Confederation Cup,Viingilio Yanga SC vs US Monastir Kombe la Shirikisho Afrika leo,Yanga vs US Monastir Leo,Yanga dhidi ya Monastir leo tarehe 19.3.2023,Yanga vs US Monastir.

VIINGILIO Yanga vs US Monastir 19 March 2023

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kuwa wanawasiliana na Matawi ya klabu ya Yanga mikoani kuandaa utaratibu wa kusafiri kuja Jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir Jumapili ya March 19, 2023 Kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari leo Jumatatu Machi 13,2023, Kamwe amesema  kuwa wanatarajia kuwa na Mashabiki wengi kutoka mikoani hivyo amewataka Mashabiki wa jijini Dar es salaam ‘wasilale’ ili kuhakikisha Jumapili uwanja wa Benjamin Mkapa unajaa.

“Tunawasiliana na Matawi ya Yanga mikoani ili kuweka sawa taratibu za safari za mashabiki kutoka mikoani wanaokuja kushuhudia mchezo dhidi ya US Monastir. Tunawaomba na wale wa Jijini Dar es salaam msilale, mechi hii ni kubwa tuhakikishe tunaujaza Uwanja wa Mkapa kuwahamasisha Wachezaji wetu waweze kushinda siku ya Jumapili,” amesema Kamwe

“Monastir tuna deni nao, na lazima tulipane. Sijui Monastir ametufungaje kule kwao. Pamoja na kutaka kufuzu lakini lazima deni lilipwe. Tunakwenda na FullHouse Full Shangwe waje tumalizane nao kwa Mkapa,” ameongeza Ali Kamwe

Aidha Ali Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo ni VIP A  itakuwa Tsh 30,000, VIP B itakuwa Tsh 20,000, VIP C itakuwa Tsh 10,000 na Mzunguuko Tsh 3,000 tu.

Tiketi tayari zimeanza kuuzwa kwenye mifumo ya ununuzi wa tiketi kwa njia ya simu na Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani.

Kamwe ametangaza kauli mbiu kuelekea mchezo huo ni FULL HOUSE, FULL SHANGWE WAJE TUMALIZANE…!

Aidha Yanga imepanga kufanya tukio kubwa la Hamasa siku ya Jumatano, Manzese Jijini Dar es salaam ambapo Wananchi watapata nafasi ya kununua tiketi na kupata Burudani kutoka kwa Wasanii mbalimbali.

Siku ya Ijumaa Yanga itaendesha zoezi la kuchangia damu Hospitali ya Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Siku ya Jumamosi, utaratibu wa ‘jogging’ kwa Wanachama na Mashabiki utaendelea kama walivyofanya katika mechi zilizopita.

Jumapili ambapo mchezo huo utapigwa kuanzia saa 9 mchana kutakuwa na parade la robo Fainali ambapo Wananchi wataandamana kutoka Jangwani kuelekea Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Yanga SC Arafat Haji ametoa tiketi 1000 za kushuhudia mchezo wetu dhidi ya US Monastir, kwa wote watakaojitokeza kwenye zoezi la uchangiaji damu litakalofanyika siku ya Ijumaa, katika Hospitali ya Mloganzila na Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani, Dar Es Salaam.

Aidha Uongozi wa Yanga unayakaribisha Makampuni/Taasisi mengine kununua tiketi kwaajili ya kuwazawadia mashujaa wote watakaojitolea damu kwaajili ya kuokoa maisha ya wengine.

Kwa maelezo zaidi piga +255 742 012 357

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *