Nijuze Habari App

VYAKULA vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Filed in Makala by on 24/03/2023 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

VYAKULA vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani

VYAKULA vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani

VYAKULA vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kipindi ambacho waumi wa dini ya Kiislamu hufunga kuanzia alfajiri hadi jioni ikitegemea na mahali ulipo.

Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan ni tendo la ibada, ambalo linawawezesha Waislamu kujiweka karibu na Mungu na kuimarisha imani yao ya kidini.

Hata hivyo, mbali na hayo, ni kipindi ambacho watu hujikuta wakila aina nyingi ya vyakula wakati wanapofungua mfungo.

Lakini je, unajua ni aina gani ya vyakula mtu aliyefunga anastahili kula?

Waathirika wa vyakula fulani

Kulingana na Dkt. Lawan Musa Tahir, wa mjini Abuja kwanza kuna wale ambao pengine ni wagonjwa wa kisukari au wenye maradhi ya ini, wanastahili kuendelea kuzingatia vyakula vyao.

Hali hii ni sawa na yeyote mwenye tatizo na chakula fulani, pengine miili yao hudhurika wanapokula vyakula fulani, hata kama umefunga mwezi wa Ramadhani, unapofungua zingatia vyakula vyako vya kila siku.

Pia kuna mazingira tofauti ya kuishi, kuna wale wanaoishi maeneo ya jua kali ambako watu wanakunywa maji mara kwa mara. Wanapofungua wajitahidi kunywa maji kwa wingi.

Orodha ya vyakula ambavyo waliofunga wanastahili kula au kutokula:

  • Epuka vyakula vyenye viungo vingi na mafuta mengi kwasababu vitaongeza kiu na joto mwilini
  • Kula vyakula vyenye majimaji hasa matunda kama vile, ndizi, nanasi, papai, matikiti maji na kadhalika
  • Kunywa maji moto kama vile chai, kakao kwa sababu inatayarisha tumbo baada ya kukaa saa nyingi bila kula chakula
  • Epuka kujaza tumbo chakula – utaona kuna watu wanaokula kupita kiasi wakati mmoja. Hilo ni tatizo. Ikiwa utafanya hivyo, mwili wako hauwezi kutumia vizuri ile nguvu au nishati ya mwili ambayo umepata kwa wakati mmoja. Hili linaweza kusababisa kuongeza uzito. Ni vyema kula kidogo kidogo kisha unapumzika ili uweze kula tena baadaye
  • Pia usivute sigara unapokuwa karibu na jamaa zako kwasababu ni hatari kwa afya
  • Hakuna tatizo lolote na kufanya mazoezi wakati wa mfungo – lakini fanya kidogo kidogo
  • Matunda yaliyokauka kama vile tende, lozi na jozi pia ni muhimu sana kupata. Zina uwezo wa kukufanya uhisi umeshiba kwa kipindi kirefu cha siku.

Unapofunga mwezi wa Ramadani, sio tu kwamba unabadilisha mfumo wako wa kula bali pia mfumo wa kulala, na pia utakuwa katika mabadiliko ya kimwili na kisaikolojia.

Pia ni vyema kufahamu kuwa mwili kutokuwa na maji ya kutosha na kukosa kula kwa wakati kama ulivyozoea, kasi ya umeng’enyaji wa chakula inapungua ili kutumia nguvu ulio nayo kwa ufasaha zaidi.

Ni wazi kwamba kipindi cha mfungo wa Ramadhani kama hiki, sio tu suala la chakula utakachokula, lakini pia kiwango cha chakula na aina ya chakula unachokula, kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha mwili unakuwa na afya njema kila wakati.

Na ili kuwa na nguvu na virutubisho vinavyohitajika mwilini kila siku, unastahili kula vyakula vyenye protini, wanga, vitamini na madini mengine, na pia unastahili kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha.

Vyakula vinavyofaa kuliwa wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaanza kuchambua kimoja baada ya kingine, Mbali na Waislamu, uchambuzi huu unawafaa pia wale ambao siyo Waislamu.

Chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Baada ya kushinda kutwa nzima na Swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo, kuhitaji kujazilizwa tena. Aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini na hasahasa ubongoni ni glukosi.

Mshuko wa sukari walioupata wale ambao hawakula au kunywa kwa kipindi kirefu, unaweza kusababisha ulegevu wa mwili.

Pindi sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha vyenyewe na kumfanya mtu aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho.

Ingawaje tende, mara nyingi, si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta, na ni chanzo madhubuti cha sukari.

Nusu ya sukari zitolewazo na tende ni kwaajili ya glukosi pekee. Usambazaji wa haraka-haraka wa glukosi itokayo kwenye tende huusaidia mwili kuodokana upesi na hali ya ulegevu kiasi kwamba mtu aliyefunga huweza kujimudu sawasawa katika ibada.

Mbali ya glukosi, tende pia ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi ambazo huwezesha michakato ya umeng’enyaji mwilini kuendelea, na huzuia tatizo la kushindikana kwa michakato hiyo ya uyeyushaji wa chakula mwilini.

Vilevile tende ni chanzo kizuri cha potasiamu, madini ambayo ni muhimu kwa usawazishaji wa maji mwilini. Hivyo, wale ambao hawapendelei ladha ya tende wanaweza kupata manufaa ya chakula hiki kwa kula angalau tende moja, na wale wanaopendelea tende, basi wanaweza kula tatu, tano, na kadhalika.

KUNYWA MAJI

Mwili wa binadamu, kwa kiasi kikubwa, unajengwa na maji. Faida za maji ni kubwa. Kama unavyohijati sukari kujirudishia nishati upesi, ndivyo unavyohitaji maji kujijazilizia ili uweze kufanya kazi vizuri.

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Siyo tu maji huurudishia mwili maji upesi na kukata kiu, bali pia ni kisafishio asilia cha uchafu na sumu ambazo zimejilimbikiza kwa muda fulani.Kwa kutwa nzima, mtu mzima mwenye afya nzuri, hushauriwa kunywa jumla ya vikombe vinane vya maji.

Hii haijumuishi yale maji yatokanayo na vyakula kama vile matunda na mboga mboga.

Kwa vile mtu aliyefunga huwa hanywi maji muda wote wa swaumu yake, basi naye anahitajika kufikisha kiwango hicho cha unywaji wa maji kabla ya daku na baada ya futari.

Inapendekezwa hivi, kwamba mwanzoni mwa kufuturu, mtu anywe kiasi kidogo cha maji (nusu kikombe au kikombe kimoja), na baada ya kufuturu, anywe maji kwa viwango vidogo muda baada ya muda (mathalani nusu kikombe au kikombe kimoja kila baada ya saa moja).

Hii itaepusha ujazo mkubwa wa maji tumboni kwa wakati mmoja na itarejesha maji mwilini kidogokidogo kabla ya swaumu inayofuata

KUNA aina sita za vyakula na ulaji ambao mfungaji anashauriwa kuepuka ili kulinda afya yake wakati huu wa mfungo wa Ramadhani, vyakula hivyo ni kama ifuatavyo:

Vyakula vya kukaanga na vyakula vya mafuta mengi kama chips, sambusa, biriyani, pilau na kadhalika vinafaa kuepukwa kwa sababu vina calories nyingi na virutubisho vichache hivyo kusababisha mlo uwe usio na uwiano.

Hii husababisha shibe isiyo na faida na huongeza uchovu wakati wa Ramadhani kwa mfungaji.

Pia mfungaji aepuke kula vyakula vilivyo na chumvi nyingi kama achari pickles, sauces, chips na kadhalika kwa sababu chumvi hunyonya maji mwilini.

Kutokana na unywaji mchache wa maji ndani ya Ramadhani, utumiaji wa chumvi nyingi unaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini, kitaalamu huitwa dehydration na udhaifu wa mwili ndani ya Ramadhani

Mfungaji pia aepuke kula vyakula na vinywaji vilivyo na sukari nyingi kama soda, pipi, vinywaji vya kuongeza nguvu n.k. Ingawa vinaweza kukupa nguvu ya haraka lakini vyakula hivi vina virutubisho hafifu sana visivyo na manufaa mwilini. Pendelea juisi ya matunda.

Chai na kahawa kupita kiasi wakati wa daku ikitumika kwa wingi ni aina ya vinywaji ambavyo huchochea kiwango kikubwa cha maji na chumvi kuchujwa kupitia njia ya mkojo.

Hii husababisha madini, maji na chumvi ambavyo vingehitajika mwilini wakati wa mchana kupotea kupitia njia ya mkojo.

Mara baada ya kula chakula wakati wa futari au daku mwili unahitaji muda kumeng’enya chakula. Subiri kwa saa mbili baada ya kula kabla hujalala.

Kula sana kunaweza kukuletea matatizo ya kimetabolitiki kama kushuka au kupanda sukari katika damu na kupungukiwa maji. Kula vyakula vilivyo na fibres (nyuzinyuzi) za kutosha wakati wa daku. Hivi ni vyakula vinavyopatikana katika

nafaka na mbegumbegu mfano mtama, matunda safi, mboga za majani na mkate wa nafaka zisizokobolewa. Unashauriwa kunywa maji mengi Ili kupunguza gesi inayoweza kuletwa na vyakula vilivyo na nyuzinyuzi (fibres). Kwa kawaida tende, maji na juisi hutumika wakati wa kufuturu.

Tumia tende tatu na juisi glasi moja ili ikusaidie  kurudisha sukari katika hali ya kawaida mwilini na kukupa nguvu ya haraka. Baada ya futari kunywa maji glasi nane kidogo kidogo kabla ya daku ili kurudisha maji mwilini.

Chagua nyama zilizo na mafuta kidogo, kama ni kuku, ondoa ngozi yake na mafuta yanayoonekana wazi kabla ya kupika nyama za aina nyingine. Ni vema kuoka au kuchoma vyakula badala ya kuvikaanga na kama utalazimika kukaanga punguza kiwango cha mafuta unayotumia.

Kula taratibu na hakikisha unatafuna chakula vizuri kabla ya kumeza, watu wengi wana tabia ya kula chakula kingi kwa haraka hivyo kusababisha matatizo ya tumbo. Kumbuka inachukua hadi dakika 20 kwa tumbo lako kuujulisha ubongo kuwa umeshiba.

Jenga tabia ya kutembea kwa angalau dakika 30 kila siku baada ya saa moja baada ya futari kwani husaidia mwili kubadilisha maji na chakula ulichokula kwa faida ya mwili. Ni vizuri chakula cha futari kikawa chepesi.

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *