Nijuze Habari

WAFUNGWA kuanza kupewa likizo

Filed in Habari by on 02/08/2022 0 Comments

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akitembelea Gereza Mkoani Kigoma

Nijuze Habari Application

WAFUNGWA kuanza kupewa likizo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akitembelea Gereza Mkoani Kigoma

WADAU wa Mahakama mkoani Kigoma wameazimia kwa pamoja kuanza kutekeleza adhabu mbadala kwa wafungwa ikiwemo kutoa likizo kwa lengo la kuwawezesha wafungwa kuandaa maisha nje ya kifungo na kuishi karibu na familia zao wakiendelea kufanya kazi za maendeleo.

 

Adhabu mbadala kwa wafungwa ikiwemo kupewa likizo itahusisha wafungwa wenye vifungo chini ya miaka mitatu hatua itakayosaidia kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani.

Wafungwa kupata likizo kurejea uraiani

Mkurugenzi Msaidizi idara ya huduma za Uangalizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze, amesema hatua hiyo itasaidia wafungwa kuzoeana na familia zao na kujiongezea kipato na kutoka vifungoni wakiwa tayari na mahusiano mazuri na familia.

Wafungwa wanatakiwa pia kufanya kazi za kijamii

Kwa upande wake Afisa Mhifadhi Wakimbizi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Mkoa wa Kigoma Rehema Msami, ambao wameratibu vikao vya kuwakutanisha wadau wa sheria mkoani Kigoma, wameomba pia wafungwa ambao ni wakimbizi kuwa sehemu ya mpango wa vifungo mbadala kulingana na sheria inavyoelekeza.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.