telegram Nijuze Habari

WALIOVUJISHA Mtihani wafikishwa Mahakamani

Filed in Habari by on 20/10/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

WALIOVUJISHA Mtihani wafikishwa Mahakamani

WALIOVUJISHA Mtihani wafikishwa Mahakamani

WALIOVUJISHA Mtihani wafikishwa Mahakamani

Walimu saba na wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kuvujisha mtihani wa Taifa wa Darasa la saba mwaka 2022.

Wakisomewa hati ya mashtaka iliyosomwa Mahakamani hapo na wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga imewataja washtakiwa hao kuwa ni Theresia Chitanda, Elinami Sarakikya, Joyce Nkomola , Lloyd Mpande, Olomy Odongo, Docras Muro na Alcherous Malinzi na
Patrick Chawawa.

Hati hiyo ya mashtaka wamesomewa Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Pamela Mazengo, ambapo imedaiwa kuwa kati ya October 02 hadi 12 mwaka huu Jijini Dar es Salaam washtakiwa, walisambaza Mtihani huo kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp na Telegram na kusababisha mtihani huo kuvuja kwa watu ambao hawakuwa na mamlaka ya kuusimamia.

Imeelezwa kuwa katika tarehe hizo hizo Jijini Dar es Salaam mshitakiwa Malinzi alitengeneza nyaraka za Uongo kuonesha kama mtihani wa Taifa wa Darasa la saba wa somo la uraia, Maadili na Maarifa ya Jamii kuwa mitihani hiyo ni ya halali na umetolewa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), wakati akijua kuwa siyo kweli.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo ambapo miongoni mwa washtakiwa hao mshtakiwa mmoja tu ‘Mpande’ ndiye amefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyokuwa yamewekwa huku wengine wote wakirudishwa mahabusu.

Mahakama imewataka washtakiwa hao kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh. Milioni tano.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika hivyo wameiomba Mahakama kuipangia tarehe nyingine kwa ajali ya kutajwa na imeahirishwa hadi Novemba 02 mwaka huu.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *