Nijuze Habari

Wanafunzi 10 Bora Matokeo ya Darasa la Saba 2021

Filed in New by on 30/10/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) leo Jumamosi October 30, 2021 limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2021 ambapo mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi St Anne Marie iliyopo mkoani Dar es Salaam, Eluleki Evaristo Haule limemtangaza ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani ya Darasa la Saba 2021.
Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo sita waliyotahiniwa.
Amemtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Happy Joseph Deus kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mkoa wa Mara na nafasi ya tatu ikienda kwa John Chacha Charles kutoka Twibhoki ya Mara pia.
Aliyeshika nafasi ya nne ni Joshua Mahende Jacob kutoka shule ya msingi Twibhoki iliyopo Mara pia, Eva Sebastian Chengula kutoka shule ya msingi Fountain of Joy ya Dar es Salaam ameshika nafasi ya tano, Joctan Samwel Matara kutoka Twibhoki ya Mara ameshika nafasi ya sita.
Barnaba Jumanne Magoto kutoka shule ya msingi Twibhoki ipo Mara pia ameshika nafasi ya saba, Rahma Ombi Juma kutoka shule ya Mtuki Highland iliyopo Dar es Salaam ameshika nafasi ya nane na nafasi ya tisa ni Juliana John Shimbala kutoka St Joseph’s nafasi ya kumi ameishika Jackline Manfredy kutoka shule ya Masaka iliyopo Dar es Salaam.
telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.