Nijuze Habari

WASHINDI wa Tuzo za CAF 2022

Filed in Michezo by on 22/07/2022 0 Comments

KIUNGO Mshambuliaji wa Klabu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika tuzo za CAF Zilizotolewa Usiku wa July 21,2022.

Nijuze Habari Application

WASHINDI wa Tuzo za CAF 2022

KIUNGO Mshambuliaji wa Klabu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika tuzo za CAF Zilizotolewa Usiku wa July 21,2022.

Sadio Mane amekuwa mchezaji wa 10 kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika zaidi ya mara moja.

Sadio Mane Senegal & FC Buryen MunichNahodha huyo wa Senegal alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo ya mwaka 2022 katika hafla ya utoaji wa tuzo za Shirikisho la Soka Afrika mjini Rabat, Morocco siku ya Alhamisi July 21, 2022.

“Nina furaha sana sana kupokea kombe mwaka huu,” Mane mwenye umri wa miaka 30, alisema alipokuwa akipokea zawadi yake.

Mane alimshinda kipa mwenzake na Chelsea, Edouard Mendy na mwenzake wa zamani wa Liverpool, Salah, ambaye timu yake ya Misri ilipoteza Fainali ya February.

Mane anakuwa mchezaji wa sita kutajwa kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka mara mbili, Wengine ni Mohamed Salah, Didier Drogba, Roger Milla, Nwankwo Kanu na El Hadji Diouf.

George Weah na Abedi Pele wote ni washindi mara tatu, huku Samuel Eto’o na Yaya Toure wakishinda tuzo hiyo mara nne kila mmoja.

Aliou Cisse SenegalTuzo ya Kocha Bora wa CAF 2022 ilienda kwa Aliou Cisse mwenye umri 46, aombaye aliiongoza Senegal kushinda kombe lao la kwanza la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon, mapema mwaka huu, baada ya kuishinda Misri kwa mikwaju ya penalti.

Cisse pia ameiongoza Simba hao wa Teranga Kufuzu kwa kombe la Dunia nchini Qatar baadaye mwaka huu mbele ya Misri katika mechi ya mchujo.

Cisse amekuwa kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Senegal tangu 2015 na aliiongoza kutinga Fainali ya AFCON mwaka 2019 kabla ya ushindi wao mwaka huu.

Cisse aliiongoza Senegal kama nahodha kwenye kombe la Dunia la 2002 huko Japan, ambapo Senegal ilifika robo Fainali ya kihistoria, Bora zaidi kuliko Taifa lolote la Afrika kuwahi kufika kwenye michuano hiyo.

Pape Ousmane Sakho Simba SCGoli Bora la Mwaka 2022 la CAF limeenda kwa Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC na Segenal, Pape Ousmane Sakho mwenye umri wa miaka 25.

Goli la tikikata alilofunga dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF, mchezo uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, ndilo limechaguliwa Goli Bora la mwaka 2022 Afrika.

Wydad Casablanca Tuzo ya Timu Bora ya Mwaka upande wa vilabu imekwenda kwa mabingwa wa Afrika, Wydad Casablanca ya Morocco.

Hii ni mara ya pili Mfululizo kwa Wydad kuchukua tuzo hii.

Mohamed El Shenawy Al Ahly SCGolikipa wa Al Ahly, Mohamed El Shenawy ndiye mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa mashindano ya vilabu ndani ya Afrika (Interclub Player Of the Year)

Pape Matar Sarr Tottenham Hotspur & SenegalPape Matar Sarr kutoka Senegal anayekiwasha Tottenham Hotspur ndiye Mchezaji Bora Chipukizi. (Young Player Of The Year)

Everyn BanduEveryn Bandu ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka 2022 kwa wachezaji wenye umri mdogo (young player of the year)

SenegalTimu ya taifa ya Senegal imeshinda tuzo ya Timu Bora kwa mwaka 2022.

Mamelodi SundownsTuzo ya Klabu Bora ya mwaka 2022 kwa upande wa Wanawake imeenda kwa Mamelodi Sundowns.

Desire Ellis Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka kwa upande wa Wanawake imeenda kwa Desire Ellis.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.