Nijuze Habari

WATATU Wafyekwa Simba, Wengine Kikaangoni

Filed in Usajili by on 29/07/2022 0 Comments

WATATU Wafyekwa Simba Wengine KikaangoniIKIWA ni takriban wiki mbili tangu kuanza kwa kambi ya mazoezi ya Klabu ya Simba SC nchini Misri, Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Zoran Maki amewaondoa Kikosini Wachezaji watatu wa Kimataifa kwa kutoridhishwa na Viwango vyao.

Nijuze Habari Application

WATATU Wafyekwa Simba, Wengine Kikaangoni

WATATU Wafyekwa Simba Wengine KikaangoniIKIWA ni takriban wiki mbili tangu kuanza kwa kambi ya mazoezi ya Klabu ya Simba SC nchini Misri, Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Zoran Maki amewaondoa Kikosini Wachezaji watatu wa Kimataifa kwa kutoridhishwa na Viwango vyao.

Meddie Kagere vs Chris Mugalu waachwa Simba SCWachezaji hao walioondolewa na kwa maana hiyo hawatakuwepo Simba SC msimu ujao wa 2022/2023 ni Washambuliaji Wawili Chriss Mugalu (DR Congo) na Meddie Kagere (Rwanda), huku Kiungo Thadeo Lwanga wa Uganda naye akijumuishwa kwenye mpango huo.Thadeo Lwanga atemwa Simba SC

Imeelezwa kuwa Zoran Maki bado hajamaliza kupitisha fyekeo lake huku ikielezwa kuwa kuwa Wachezaji wengine watatu wanaweza kufuata mmojawapo akiwa ni nyota mpya kabisa aliyesajiliwa msimu huu.

Kocha Zoran alipewa jukumu hilo na Uongozi wa Simba SC, ili kubaki na idadi kamili ya wachezahi 12 wa Kigeni, ambao wanatakiwa kusajiliwa Kikanuni katika Ligi ya Tanzania Bara.

WATATU Wafyekwa Simba Wengine KikaangoniBaada ya Kikosi cha Simba SC kupoteza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Haras El Hodoud juzi Jumatano July 27,2022, Zoran aliwapa taarifa mabosi wa klabu hiyo akiwaambia hatakubaliana na ubora wa washambuliaji Chris Mugalu na Meddie Kagere.

Mbali na Mugalu na Kagere ambao ndio walikuwa washambuliaji wawili pekee wa Kigeni walioitumikia Simba SC msimu uliopita, pia akakata jina la kiungo Thadeo Lwanga.

Tayari Wachezaji hao wameshaondoka kambini Misri na kurejea Jijini Dar es salaam kwaajili ya kumalizana na mabosi wa Simba SC.

Habari njema kwa Simba ni kwamba kiungo Sadio Kanoute ambaye alikwama kujiunga na kambi kutokana na pasi yake kujaa yuko katika hatua za mwisho kujiunga na wenzake akisubiri visa pekee, Kanoute tayari ameshatua Tanzania akisubiri taratibu za safari.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.