Nijuze Habari App

YANGA, GSM zasaini Mkataba mnono wa udhamini

Filed in Michezo by on 12/09/2022 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


 

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

YANGA, GSM zasaini Mkataba mnono wa udhamini

YANGA, GSM zasaini Mkataba mnono wa udhamini

YANGA vs GSM

KLABU ya Yanga na kampuni ya GSM zimesaini Mikataba Minono ya udhamini na Utengenezaji wa Jezi kwa kipindi cha miaka mitano.

Mkataba wa Utengenezaji wa Jezi na Vifaa vya Michezo vyenye Nembo ya Klabu ya Young Africans SC wenye thamani ya Tsh Bilioni 1.5 kwa mwaka, utaingizia Yanga Tsh Bilioni 9.1 katika kipindi chote cha miaka mitano

Mkataba wa udhamini kupitia GSM foam/Max wenye thamani ya Tsh Milioni 300 kwa mwaka utaiingizia Yanga Tsh Bilioni 1.8 katika kipindi chote cha miaka mitano.

YANGA, GSM zasaini Mkataba mnono wa udhamini

YANGA SC V GSM GROUP

Mikataba yote miwili ina thamani ya TSh Bilioni 10.9

Akizungumza katika hafla ya Utiaji saini uliofanyika kwenye Hotel ya Serena mapema leo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema kuwa Mahusiano mazuri kati ya Yanga na GSM yamepelekea kusainiwa kwa mikataba hiyo.

YANGA, GSM zasaini Mkataba mnono wa udhamini

Hersi Said Rais wa Yanga

Akizungumzia makubaliano hayo Rais wa Young Africans SC Eng.Hersi Said amesema “Tunayo furaha kubwa kuingia makubaliano haya mapya na wenzetu wa GSM, moja ya ajenda zangu katika Uongozi wangu ilikuwa ni kuipa Klabu uimara wa kiuchumi ili tuweze kujitegemea na mikataba kama hii inaiongezea Klabu thamani na kuiimarisha kimapato, na kama tujuavyo uendeshaji wa vilabu vyetu kunahitaji uiamara wa kiuchumi”

Hersi amemshukuru Rais wa Makampuni ya GSM Ghalib Said Mohammed kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya Yanga tangu tangu nyakati ngumu

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Hersi pia amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuiunga mkono GSM kwa kununua bidhaa zao mbalimbali.

YANGA, GSM zasaini Mkataba mnono wa udhamini

Bw. Allan Chonjo Mkurugenzi wa Biashara GSM

Naye Mkurugenzi wa Biashara toka GSM Group Bw. Allan Chonjo amesema. “GSM imeona Matunda makubwa sana baada ya kuingia mkataba na Club Kubwa ya Yanga na hivyo tumevutiwa na kuamua kuendelea kuwekeza kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia  msimu huu wa 2022/23 mpaka 2026/27 kwenye mikataba yote miwili yenye Jumla ya thamani ya Zaidi Tsh Bilioni 10.9.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *