Nijuze Habari

YANGA, Jackson Group zasaini mkataba mnono

Filed in Michezo by on 19/08/2022 0 Comments

YANGA, Jackson Group zasaini mkataba mnonoKLABU ya Yanga imetangaza kuingia mkataba na Jackson Group Company kampuni inayohusika na masuala ya Masoko (Marketing).

Nijuze Habari Application

YANGA, Jackson Group zasaini mkataba mnono

YANGA, Jackson Group zasaini mkataba mnonoKLABU ya Yanga imetangaza kuingia mkataba na Jackson Group Company kampuni inayohusika na masuala ya Masoko (Marketing).

Yanga na Jackson Group, zimesaini Mkataba wa miaka miwili unaolenga kuinufaisha Yanga SC, kwani Kampuni hiyo itakuwa na jukumu la Kuiendesha na Kuisimamia Yanga kwenye masuala ya Digital, Marketing, Branding nk huku ukifungua fursa zaidi kwa Wawekezaji na Wadhamini.

Jackson Group ambayo ipo chini ya Kelvin Twissa imewahi kuwezesha dili la Kampuni ya Vodacom kuidhamini Ligi kuu Tanzania Bara pia ikifanya vizuri na vilabu kama Arsenal FC, Hull City, Gor Mahia na Simba SC.

Hayo ni Mapinduzi Makubwa kwenye eneo la Uendeshaji wa Klabu hususani Kitengo cha Masoko, kwa miaka mingi Uwekezaji Mkubwa kwenye upande wa Michezo umekuwa ukielekezwa zaidi kwenye eneo la Ufundi, eneo la Utawala huku Upande wa Uendeshaji umekuwa haupewi kipaumbele.

Rais wa Yanga Hersi Said akizungumza na wanahabari wakati wa kusaini mkataba huo, amesema kuwa Kuliko kumuajiri Mkurugenzi wa Masoko Klabu imeona ni vyema ikatafuta Kampuni ya Masoko ambapo Jackson Group baada ya kukidhi vigezo vyote na taratibu hivyo Klabu imewapa kazi hii.

Kazi kubwa ya Jackson Group ni kuitafutia Klabu hiyo Masoko na Kutanua wigo zaidi wa Kibiashara.

Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said.

Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said.

“Ajenda moja wapo wakati nilivyoingia madarakani ilikuwa ni kutengeneza mfumo ambao utakwenda kuifanya klabu hii kuwa moja ya vilabu vikubwa Barani Afrika, tulio la kusaini Mkataba na JACKOSN GROUP unaakisi uelekeo wa imara wa kifedha wa Klabu kwa kuleta wadhamini zaidi kwenye Klabu yetu kupitia kampuni hii ambayo ina uzoefu mkubwa katika sekta hiyoRais wa Young Africans SC Hersi Ally Said.

“Kampuni ya Jackson Group ni kampuni ya Watanzania wenzetu ikiendeshwa na CEO Guru katika maswala ya kibiashara na masoko Bw. Kelvin Twissa historia yake inajieleza ni mtu wa namna gani katika Uwanja huu wa Masoko Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said.

  • Mambo matano (5) muhimu ya kufahamu kwenye mkataba kati ya Yanga na Jackson Group:Yanga SC na Jackson Group

1️⃣Mkataba ni wa mahusiano ya kibiashara na masoko.

2️⃣Mkataba huu ni wa Utekelezaji wa mfumo wa Mabadiliko kwenye idara ya Masoko kama ilivyoshauriwa Laliga.

3️⃣Jackson Group itafanya kazi chini ya Secretariat ya Yanga kwa kuzingatia miongozo, sera na tamaduni za Yanga.

4️⃣Mkataba huu ni wa kimahusiano, hauna thamani ya kifedha, pande zote zitafaidika pale Biashara itakapopatikana.

5️⃣Mkataba ni wa miaka miwili (2).

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.