Nijuze Habari

YANGA kuanzia hatua ya awali CAF Champions League

Filed in Michezo by on 07/06/2022 0 Comments

YANGA kuanzia hatua ya awali CAF Champions LeagueSHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa Klabu ya Young Africans itaanzia hatau ya awali ya Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika msimu ujao wa 2022/2023.

Nijuze Habari Application

YANGA kuanzia hatua ya awali CAF Champions League

YANGA kuanzia hatua ya awali CAF Champions LeagueSHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa Klabu ya Young Africans itaanzia hatau ya awali ya Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika msimu ujao wa 2022/2023.

CAF imethibitisha uratibu huo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kuweka Video inayoonyesha Mshambuliaji wa klabu hiyo Fiston Mayele akiwasalimia mashabiki walipokuwa njiani.

Young Africans itashiriki Michuano hiyo, kufuatia kuwa na uhakika wa kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, huku ikibakisha alama tatu kufikia lengo hilo.

Katika hatua nyingine CAF imesisitiza klabu zote ambazo zitashiriki michuano ya Kimataifa kuhakikisha zinawasilisha mapema orodha ya majina ya wachezaji watakaosajiliwa kwaajili ya michuano hiyo.

Msimu uliopita Young Africans ilishiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lakini ilitolewa katika hatua ya awali kwa kufungwa jumla ya mabao 2-0 na Rivers United ya Nigeria.

Aidha msimu ujao Tanzania itawakilishwa na timu mbili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na mbili nyingine zitashiriki michuanio ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.