YANGA Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Msimu wa 2022/23

Filed in Michezo by on 13/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

YANGA Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Msimu wa 2022/23

YANGA Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Msimu wa 2022/23

YANGA Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Msimu wa 2022/23

 

Klabu ya Young Africans imeweka rekodi ikitwaa Ubingwa wa 29 Ligi Kuu Bara ikiifunga Dodoma Jiji mabao 4-2 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Young Africans yamefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 38, Mudathir Yahya akifunga mawili dakika ya 70, 90 na Farid Mussa dakika ya 88.

Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Collins Opare dakika ya 59 huku la pili likifungwa na Seif Karihe dakika ya 67.

Ubingwa huu kwa Yanga ni wa 29 kuuchukua tangu ilipochukua mara ya kwanza mwaka 1965 ikiwa ndio vinara na kufuatiwa na Simba SC waliochukua mara 22.

June 15, 2023, Young Africans ilitangaza Ubingwa wake wa 28 katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya Ushindi wa Mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo Young Africans ilitangaza Ubingwa huo baada ya kufikisha pointi 67 tena bila ya kupoteza kufuatia kucheza michezo 27 kwa mabao yaliyofungwa na Mshambuliaji, Fiston Mayele aliyefunga mawili na Chico Ushindi.

Katika michezo 28 ambayo Yanga imecheza imeshinda 24, sare miwili na kupoteza miwili ikiendelea kuongoza Ligi Kuu Bara na pointi 74.

Takwimu za Msimu 2021-2022
-Michezo 28
-Alama 73

Takwimu za Msimu wa 2022-2023
-Michezo 28
-Alama 74

Klabu hiyo inatatajiwa kusafiri kwenye Afrika Kusini kwaajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants saa 10 alfajiri ya kesho Jumapili.

Katika hatua nyingine Bodi ya Ligi Kuu imeipongeza klabu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya NBC kwa msimu wa 2022/23

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *