Nijuze Habari

YANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa Udhamini

Filed in Michezo by on 27/07/2022 0 Comments

YANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa UdhaminiKLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani ya Tsh 12.3B kwa miaka mitatu (3), ambayo ni sawa na 4.1B kwa kila mwaka.

Nijuze Habari Application

YANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa Udhamini

YANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa UdhaminiKLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani ya Tsh 12.3B kwa miaka mitatu (3), ambayo ni sawa na 4.1B kwa kila mwaka.

Hili ni ongezeko la Tsh bilioni 2 kwa mwaka kutoka kwenye mkataba awali wa bilioni moja kwa mwaka mmoja.

YANGA na Sportpesa zasaini Mkataba mpya wa Udhamini

Aidha Tarimba amesema kuwa Sambamba na Fedha hizo ambazo Yanga itavuna, pia Bonus zitatolewa kama ilivyoainishwa kwenye mkataba ambapo Yanga ikifanikiwa kuwa Bingwa wa Ligi Kuu atapata Bonus ya 150M.

Yanga ikifanikiwa Nusu Fainali Azam Sports Federation Cup (ASFC) itapata Bonus ya 75M na endapo itakuwa Bingwa (ASFC) itapata 112M.

Mkataba wa awali kati ya Yanga SC na Sportpesa ulikuwa wa miaka mitano (5) wa Tsh 5.B sawa na Tsh 1 Bilioni kila mwaka katika kipindi chote cha mkataba yaani miaka mitano (5).

Mkataba mpya wa Udhamini Mkuu wa Yanga SC vs SportPesa TanzaniaRais wa Young Africans SC Eng. Hersi Said na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Ndg. Tarimba Abbas wakionyesha makubaliano ya mkataba mpya kati ya SportPesa na Young Africans SC.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tarimba Abbas TarimbaAkiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tarimba Abbas Tarimba amesema Kampuni ya Sportpesa ndiyo Kampuni pekee ya michezo ya kubashiri iliyosaidia kwa kiasi kikubwa kusaidia vilabu vya Simba na Yanga kujiimarisha kiuchumi kupitia udhamini wao lakini pia kupitia mashindano ya Sportpesa tangu mwaka 2017.

Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi SaidKwa upande mwingine Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said ameipongeza Kampuni ya Sportpesa chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Abbas Tarimba kwa kufikia makubaliano hayo ya kihistoria kwa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani huku akiahidi kusimamia maelekezo na makubaliano ya mkataba huo na kusisitiza kuwa Yanga ipo tayari kufanya mambo makubwa zaidi na SportPesa.

Rais wa Young Africans SC Eng.Hersi Said, CEO Senzo Mbatha pamoja na Wachezaji wakipokea hundi ya Tshs.Milioni 100Rais wa Young Africans SC Eng.Hersi Said, CEO Senzo Mbatha pamoja na Wachezaji wakipokea hundi ya Tshs.Milioni 100 kwa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Ndg.Tarimba Abbas kama sehemu ya Bonus baada ya kushinda Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2021/2022.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.