Nijuze Habari

YANGA yaachana na Bumbuli, mwenyewe afunguka, Mrithi wake atajwa

Filed in Michezo by on 12/08/2022 0 Comments

Hassan Bumbuli Yanga SCUONGOZI wa Klabu ya Yanga SC, umethibitisha kuachana na aliyekuwa Afisa Habari na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndugu Hassan Bumbuli baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Nijuze Habari Application

YANGA yaachana na Bumbuli, mwenyewe afunguka, Mrithi wake atajwa

Hassan Bumbuli Yanga SCUONGOZI wa Klabu ya Yanga SC, umethibitisha kuachana na aliyekuwa Afisa Habari na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndugu Hassan Bumbuli baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Yanga imetoa Shukrani kwa Utumishi wake na kusema kuwa Bumbuli amemaliza mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo, hivyo uongozi unamshukuru sana kwa kazi yake nzuri na kumtakia kila la kheri na mafanikio katika maisha na kazi zake nje ya Klabu ya Yanga.

Baada ya kuachana na Yanga Bumbuli kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika kuwa; Kwa dhati ya moyo Wangu NAWASHUKURU sana Wana Yanga.

Hassan Bumbuli Yanga SCHakika naweza kusema kwamba ni ninyi ndio mnafanya ukubwa huu Klabu ya Yanga.

Inaweza kuhuzunisha kwamba leo nawaaga, naondoka uongozini, lakini nina furaha na shauku kwa changamoto mpya mbele yangu, na pia nina shauku kuona mpya yaliyoandaliwa kwaajili yenu na kwa Klabu yangu pendwa.

Ni zawadi nzuri sana niliyopokea na kuifurahia kufanya kazi Yanga, kuwahudumia Wananchi.

Ahsanteni kwa kunionyesha wema na hekima, hakika mlifanya Yanga kuwa mahali nilipofurahia sana kutumia muda wangu za kazi na zaidi.

Kwenu WanaYanga, sina la kusema, hii ni kwa sababu sipati maneno ya kuelezea jinsi ninavyowashukuru!

Ninyi ni watu Maalum sana. Nimekuja tukiwa watupu vyote pesa na mataji, naondoka huku vikapu vikiwa vimesheheni na rekodi iliyowekwa kwa kishindo.

Ahsanteni kwa kunipa nafasi ya kuwatumikia alimaliza Hassan Bumbuli.

Ali Kamwe Yanga SCKatika hatua nyingine, baada ya mchakato wa kumsaka mrithi wa Bumbuli kuanza, mchambuzi wa Azam TV Ali Kamwe ametajwa kuwa miongoni mwa wanaowania Ukuu wa Kitengo hicho cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Yanga SC.Ali Kamwe Yanga SC

Kamwe anawania kurithi mikoba iliyoachwa na Hassan Bumbuli ambaye mkataba wake umefikia tamani Leo Ijumaa August 12,2022.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.