YANGA yaanza safari ya kurejea Tanzania

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


YANGA yaanza safari ya kurejea Tanzania

YANGA yaanza safari ya kurejea Tanzania
BAADA ya Ushindi wa Mabao 2-1 dhidi ya Marumo Gallants na kufanikiwa Kufuzu hatua ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, kikosi cha Yanga kimeondoka Mjini Rustenburg mapema leo kuelekea Johanesburg, Afrika Kusini.
Yanga inaondoka Afrika Kusini leo kurejea nyumbani Tanzania ambako Jumapili hii ya May 21 itakuwa na mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida Big Stars ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida Kuanzia Saa 9:30 Alasiri.
Afisa Habari wa Klabu hiyo, Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuiunga mkono timu yao ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya Msimu huu.
Kamwe amesema kuwa huu sio wakati wa Shamrashamra, kwani wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya Singida BS na kutinga Fainali ya Azam Sports Federation Cup 2023.
“Nawaambia Wanachama na Mashabiki wetu, waendelee kutuunga mkono, muda wa Shamrashamra bado, wasije Uwanja wa ndege kutupokea kwani bado hatujamaliza kazi, tunakabiliwa na mechi mbili muhimu ambazo ni Nusu Fainali ya FA na Fainali ya Shirikisho Afrika,” alisema Kamwe
Yanga baada ya kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itacheza na USM Alger ya Algeria kwenye Fainali ambayo inachezwa nyumbani na Ugenini na mchezo wa Kwanza utapigwa Jijini Dar es salaam May 28, huku mchezo wa Pili ukitarajiwa kupigwa June 3 mwaka huu nchini Algeria.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024
- YANGA yashika Nafasi ya 9 Simba ya 10 Afrika 2022/2023
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.