YANGA yaifuata Marumo Gallants South Africa

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


YANGA yaifuata Marumo Gallants South Africa

YANGA yaifuata Marumo Gallants South Africa
BAADA ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, kikosi cha Young Africans kimeondoka nchini Alfajiri ya leo Jumapili kuelekea Afrika Kusini, kwaajili ya mchezo dhidi ya Marumo Gallants ya nchini humo.
Mchezo huo wa mkondo wa Pili wa Nusu Fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika unatarajiwa kupigwa Jumatano ya May 17,2023 kuanzia 1:00 Usiku katika dimba la Royal Bafokeng nchini Afrika Kusini.
Katika mchezo wa mkondo wa Kwanza uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, wenyeji Yanga walifanikiwa kuibuka na Ushindi wa mabao 2-0.
Kuelekea mchezo huo Yanga inahitaji Ushindi wa aina yoyote au sare yoyote ili Kufuzu Fainali ya CAF Confederation Cup 2022/2023.
Katika hatua nyingine, Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika juhudi za hamasa kuendelea kuunga mkono michezo nchini hususani katika mashindano ya kimataifa, imegharamia jumla ya mashabiki 55 watakaosafiri kuelekea nchini Afrika Kusini, kwenda kuishangilia klabu ya Yanga
Ni katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants, utakaopigwa tarehe 17 Mei, 2023 kwenye uwanja wa Royal Bafokeng uliopo katika mji wa Rustenburg nchini humo
Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari jana Mei 13, katika ukumbi wa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
Yakubu alisema msafara huo wa hamasa utaongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma
“Katika hii safari, Serikali imesaidia Yanga kupeleka baadhi ya mashabiki 55 ambao wataondoka kesho (leo) jumapili tarehe 14 Mei, 2023 kueleka Afrika Kusini na huko wataungana na Watanzania waishio Afrika Kusini katika kuhakikisha wanatoa hamasa ya kutosha”
“Nimeongea na Balozi, wao pia wamejiandaa kuwapokea lakini pia wameandaa mabasi kutoka kila mji kuhakikisha Watanzania wanakuwa wengi katika mchezo huo,”alisema Yakubu.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga, Andrew Ntime alisema kuwa wao kama timu wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo huku akiishukuru serikali kutokana na mchango wake wa kupeleka mashabiki hao
Msafara wa Yanga umeondoka nchini Alfajiri ya leo Jumapili kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Jumatano.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.