Nijuze Habari App

Yanga yaingiza Bilioni 17 msimu wa 2022/2023

Filed in Michezo, New by on 24/06/2023 0 Comments
Share This

SHINDA 50,000 BURE KILA SIKU BONYEZA HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Yanga yaingiza Bilioni 17 msimu wa 2022/2023

Yanga yaingiza Bilioni 17 msimu wa 2022/2023, KLABU ya Yanga msimu wa 2022-2023 imeingiza jumla ya Sh. Bilioni 17.8 kutokana na mapato mbalimbali, ikiwemo udhamini wao kutoka makampuni ya SportPesa, Azam Media Limited, Haier, GSM Group, Jembe Energy, CRDB Bank, Unicef, Smile na Robbialac.

Hayo yamesemwa na Rais wa Yanga, Mhandishi Hersi Ally Said katika Mkutano Mkuu wa mwaka klabu uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Young Africans SC Arafat Haji

Makamu wa Rais Young Africans SC Arafat Haji

Hersi amesema kuwa katika fedha hizo, matumzi ya klabu ni Bilioni 17.3, maana yake Faida ambayo wamevuna kutokana na wadhamini ni Sh. Milioni 500.

Aidha, Rais Hersi amesema kuwa msimu wa 2022-2023 klabu hiyo pia imevuna kiasi cha Bilioni 3.5 kutokana na zawadi za ushiriki wao kwenye mashindano mbalimbali na kwamba kwa msimu ujao Bajeti yao ya matumizi itakuwa zaidi ya Sh. Bilioni 20.

Pamoja na kutwaa Ngao ya Jamii, Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Yanga ilishika nafasi ya pili Kombe la Shirikisho Afrika.

Makombe yote matatu na medali ya Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2022-23 yametambulishwa rasmi kwa Wanachama

Makombe yote matatu na medali ya Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2022-23 yametambulishwa rasmi kwa Wanachama

Rais Hersi pia amesema kuwa Uongozi wake umedhamiria kujenga Uwanja wa kisasa katika makao Makuu ya klabu, Mtaa wa Jangwani ambao utakuwa na uwezo wa kuingiza watu 15,000 hadi 18,000.

Muonekano wa Uwanja wa Klabu yetu ambao unatarajia kujengwa katika Makao Makuu ya Young Africans SC Jangwani kwenye eneo la Uwanja wa Kaunda ukitarajiwa kubeba mashabiki 15,000 hadi 18,000, NMB Yanga Stadium

NMB Yanga Stadium

“Katika uongozi wangu, mimi na wenzangu hatutamaliza muda wetu mpaka tumalize ujenzi huu wa Uwanja,” amesema Rais Hersi.

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Katika Mkutano huo pia wametambulishwa Wajumbe wapya wa Baraza la Wadhamini wa Yanga wakiongozwa na mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa kwanza wa Bara la Mapinduzi, marehemu Abeid Amaan Karume, Mama Fatma Karume.

Wajumbe wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Newala, Kapteni Mstaafu George Mkuchika, Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi, Dk Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Kinondoni, Tarimba Abbas na Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Young Africans SC

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Young Africans SC

 

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *