YANGA yakumbana na Rungu la CAF kisa Rivers United

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


YANGA yakumbana na Rungu la CAF kisa Rivers United

YANGA yakumbana na Rungu la CAF kisa Rivers United
KLABU ya Young Africans, imetozwa Faini ya Jumla ya Dola 35,000 na CAF ambayo ni zaidi ya Sh 82 milioni kwa makosa mbalimbali yanayodaiwa kufanywa katika mechi yao ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.
Malalamiko yao kwenda CAF ilikuwa gari lao kuvunjwa vioo na kuibiwa dola 5,000 huku wakidai pia kupuliziwa dawa.
Rivers walitoa Malalamiko hayo siku moja kabla ya mchezo huo uliofanyika April 30,2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, baada ya kumaliza mazoezi yao uwanjani hapo.
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), iliyokutana May 4 mwaka huu imeipiga faini Young Africans kwa madai ya kuhusika kuwasha vitochi na kupiga mafataki Uwanjani ambapo Faini yake ni dola 10,000.
Faini nyingine ni Dola 25,000 kwa madai ya kupuliza dawa kwenye gari la timu ambalo walilitumia Rivers United walipokuwa mazoezini na kuelekeza Yanga kulipa fedha hizo ndani ya siku 60 tangu kutolewa kwa adhabu hiyo.
Young Africans imepewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku tatu tangu kutolewa kwa adhabu hiyo na wakishindwa kukata rufaa ndani ya muda elekezi basi watatakiwa kulipa faini hiyo kama walivyoelekezwa.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.