telegram Nijuze Habari

YANGA yamkana Mwinyi Zahera

Filed in Michezo by on 20/10/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

YANGA yamkana Mwinyi Zahera

YANGA yamkana Mwinyi Zahera

YANGA yamkana Mwinyi Zahera

AFISA Habari wa Klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe amethibitisha kuwa mkataba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka la vijana na Wanawake, Mwinyi Zahera umemalizika tangu September 30, 2022.

Kocha huyo wa zamani wa Klabu hiyo amekuwa akipita katika vyombo mbalimbali vya habari kuzungumza masuala yanayoihusu Klabu ya Yanga SC.

Kamwe amewataka waandishi wa habari wanaomualika katika vipindi vyao wamuulize mafanikio gani ameiletea klabu ya Yanga wakati akiwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka la vijana na Wanawake na sio kuzungumzia unene wa Wachezaji.

YANGA yamkana Mwinyi Zahera

YANGA yamkana Mwinyi Zahera

Kupitia mtandao wake wa Kijamii, Al Kamwe amesema kuwa, Naheshimu sana wasifu wa Mwinyi Zahera.. Ni kocha mkubwa. Naheshimu pia maoni yake kama Mtaalam wa soka.

Lakini ndugu zangu Waandishi wa Habari nafikiri kuna jambo mnatakiwa kulifahamu.

Zahera sio mwajiriwa wa Yanga. Mkataba wake ulishamalizika tangu September 2022.

Akiwa Yanga, alikuwa na Cheo cha Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka la vijana na Wanawake.

Nafikiri kwa kujenga zaidi, kabla Zahera hajaanza uchambuzi wake wa unene wa Wachezaji, ni vyema mkaanza kwa kumuuliza kwenye majukumu yake.

Kwa nafasi yake, kwenye soka la vijana ameacha mafanikio gani kwa Yanga?

Kwenye Soka la Wanawake pia amefanya nini kwa Yanga Princesses?

Changamoto gani alipata? Nini alifanya kama mtaalamu ili kuzitatua? Nafikiri haya ni maswala ya msingi kabisa ambayo Zahera anatakiwa kuulizwa na kuyajibia kwa sasa.

Narudia tena, Naheshimu maoni yake kama mtaalamu wa soka Lakini msiruhusu akaruka hatua muhimu.

Hii itasaidia wasikilizaji wenu na mashabiki wa soka kupata maarifa zaidi.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *