Nijuze Habari

YANGA yamtambulisha mchezaji mpya kutoka Zambia

Filed in Usajili by on 16/06/2022 0 Comments

YANGA yamtambulisha mchezaji mpya kutoka ZambiaKLABU ya Yanga imeendelea kuboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa 2022/2023 baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chief ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo mwaka 2019 akitokea ZESCO United ya kwao Zambia

Nijuze Habari Application

YANGA yamtambulisha mchezaji mpya kutoka Zambia

YANGA yamtambulisha mchezaji mpya kutoka ZambiaKLABU ya Yanga imeendelea kuboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa 2022/2023 baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chief ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo mwaka 2019 akitokea ZESCO United ya kwao Zambia

Mabingwa hao wapya msimu huu wa 2021/2022 wameshinda kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji huyo wakiizidi ujanja na mbinu zote ZESCO United FC na kumnasa Mzambia huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa mkataba wa miaka miwili.

YANGA yamtambulisha mchezaji mpya kutoka ZambiaUjio wa nyota huyo unaongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji la timu hiyo kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao inayoongozwa na Fiston Mayele mwenye mabao 16 kwenye Ligi Kuu Bara mpaka sasa.

Kambole aliibukia Konkola Mine Police mwaka 2011, kabla ya kuhamia Konkola Blades mwaka 2013 ambako alicheza hadi 2014 alipokwenda ZESCO United – na tangu mwaka 2018 amekuwa akichezea timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo).

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

telegram Nijuze Habari

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.