YANGA yamtangaza CEO mpya

Filed in Michezo, Usajili by on 27/09/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

YANGA yamtangaza CEO mpya

Klabu ya Yanga imemtangaza Mzambia Andre Mtine kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akichukua mikoba ya Senzo Mbatha Mazingisa aliyeondoka klabuni hapo miezi iliyopita baada ya mkataba wake kufikia kikomo.

Utambulisho wa Mtendaji huyo mpya, umefanywa na Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said ambaye amesema wanaamini kuwa uzoefu wa Mtine utaongeza thamani ndani ya Klabu hiyo na kuleta Mafanikio ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

”Huu ni muendelezo wa ajenda yangu kubwa katika uongozi wangu ambayo ni kuimarisha kila idara kwa kuleta watu wenyewe weledi wa kufanya kazi za Yanga” amesema Hersi Said.

YANGA yamtangaza CEO mpya

Andre Mtine CEO mpya Yanga SC

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu huyo mpya Andre Mtine amesema amejiunga na Yanga kwa kuwa ni klabu kubwa na yenye historia Barani Afrika huku akitoa rai kwa Wanachama na Mashabiki wa Klabu hiyo Kushirikiana ili kusaidia kufikia malengo Makubwa ya Klabu.

“Yanga ni timu kubwa sana, nimekuwa naifuatilia kwa muda sasa. Nimejifunza kuwa ni timu kubwa, na tunaweza kuifanya kuwa kubwa zaidi, siyo tu ukanda wa Afrika Mashariki bali kuwa klabu kubwa zaidi Afrika,” amesema Mtine.

Mzambia huyo Andre Mtine alianza kujihusisha na michezo tangu mwaka 1988 na kupita klabu kama Zesco, Power Dynamo, Bidco pamoja na TP Mazembe aliyodumu nayo kwa miaka 12 sambamba na kushika nafasi ya ujumbe wa kamati ya Fedha ndani ya CAF.

Tazama CV ya Andre Mtine CEO mpya wa Yanga SC.

PARMATCH Kumwaga Mamilioni kwa Wateja Wapya | Jisajili hapa Kushinda Zawadi

PARMATCH Kumwaga Mamilioni kwa Wateja Wapya

BETI NA PARMATCH USHINDE MAMILIONI

Kampuni ya Michezo ya KUBETI na KASINO za Mtandaoni Tanzania PARMATCH imezindua Ofa mpya ya Bonasi kwa Wateja wapya.

Kila mteja mpya atakayejisajili na PARMATCH atajinyakulia BONASI sawa na kiasi alichoweka kwa mara ya kwanza kuanzia Shilingi 1,000 hadi milioni moja kwa kila mteja.

Akizungumza katika uzinduzi wa BONASI hiyo Afisa Masoko wa Parmatch amesema kuwa Bonasi hiyo itawahusu wateja wapya watakaojisajili na kuweka salio kwenye akaunti zao.

Ili uweze kujisajili na PARMATCH unatakiwa kutembelea tovuti yao kwa kugusa HAPA Kisha Jisajili.

Kujiunga na PARMATCH na kupata Bonasi ya hadi 1,000,000 (Milioni Moja) Ukideposit salio kwenye akaunti yako Bofya HAPA.

Unaweza kupata Taarifa hii kwa undani zaidi kwa kubofya Parmatch.co.tz

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *