Nijuze Habari

YANGA yasitisha safari ya Uturuki

Filed in Michezo by on 15/07/2022 0 Comments

YANGA yasitisha safari ya UturukiUONGOZI wa Klabu ya Yanga SC umethibitisha kufuta safari yao ya kwenda nchini Uturuki Kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao (Pre-season) na sasa Yanga wamepanga kwenda mkoani Morogoro kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Nijuze Habari Application

YANGA yasitisha safari ya Uturuki

YANGA yasitisha safari ya UturukiUONGOZI wa Klabu ya Yanga SC umethibitisha kufuta safari yao ya kwenda nchini Uturuki Kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao (Pre-season) na sasa Yanga wamepanga kwenda mkoani Morogoro kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Pamoja na kufuta safari ya kwenda Uturuki kampuni ya ENDA TOUR imepanga kuwashitaki klabu ya Yanga kwa TFF na FIFA ili kudai fidia ya milioni 200 kwa klabu hiyo kwa kukiuka makubaliano ya kimkataba waliyokubaliana hapo awali.

Inadaiwa kuwa klabu ya Yanga waliingia mkataba wa makubaliano na Kampuni hiyo ili waandaliwe kambi ya mazoezi (Hoteli, Viwanja) na mechi za kirafiki wakati wakiwa Uturuki kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao (Pre-season).

Yanga walipanga kuanza kambi hiyo tarehe 15/07/2022 hadi 04/08/2022.

Abbas Tarimba SportPesaKatika hatua nyingine, baada ya miaka mitano ya Udhamini wa Sportpesa, Klabu ya Yanga inatarajiwa kusaini mkataba mwingine wa miaka mitano kuendelea na udhamini wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa Utawala SportPesa Abbas Tarimba, amesema Mkataba ambao watasaini na Yanga utaweka rekodi kwani hakuna Klabu yoyote hapa Tanzania iliyowahi kupata Mkataba wa aina hiyo.

“Ni kweli mkataba tuliosaini awali umemalizika, Hivi karibuni tutaingia mkataba mwingine mkubwa zaidi na wa kihistoria na klabu ya Yanga SC, ambao haujawahi kuingiwa na klabu yoyote,” alisema Tarimba

Aidha Abbas Tarimba alithibitisha kumaliza mkataba uliodumu kwa miaka mitano baina ya SportPesa na Simba SC, na Kuitakia kila la kheri klabu hiyo.

Tarimba alisema pande zote zimeridhika kwa huduma iliyotolewa kwa kipindi chote na wanaamini Simba SC itaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika udhamini uliokuwepo kati yao.

Aliongeza kuwa wanajivunia mafanikio makubwa waliyoyapata wakiwa na Klabu ya Simba SC, na hata upande wa Klabu hiyo ana uhakika utakuwa umefurahia kufanya kazi na kampuni hiyo ya Michezo ya kubashiri nchini.

“Ni kweli tumemaliza Mkataba wa Simba SC, tumekuwa nao kwa kipindi Kirefu, sisi tulikua na matarajio ambayo tulipenda yafanyike na wao ilikua hivyo pia,”

“Naweza kusema kwamba tuheshimu maamuzi yaliyofikiwa na pande zote mbili, tunaitakia kila la kheri Simba SC katika mpango wake ndani na nje ya uwanja.” amesema Tarimba

Katika mkataba uliopita, Yanga na Simba zilikuwa zikipokea takribani Tsh Bilioni 1 kila mwaka kutoka SportPesa.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.