Nijuze Habari App

YANGA YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA 2023

Filed in Michezo by on 17/05/2023 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


 

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

YANGA YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA 2023

KLABU ya Young Africans, imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Marumo Gallants, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng NW Jijini Rustenburg nchini Afrika Kusini.

Bao la Kwanza kwenye mchezo huo lilifungwa na Fiston Mayele dakika ya 45, kabla ya Kennedy Musonda kufunga la pili dakika ya 62, huku Ranga Chivaviro akiifungia Marumo Gallants bao pekee dakika ya 90.
Bao la Ranga Piniel Chivaviro lilifanya kufungana na Fiston Mayele kwenye chati ya Ufungaji kwenye Kombe la Shirikisho Afrika 2023 kila mmoja akiwa na mabao 6.
Young Africans inatinga Fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 kufuatia Ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Kwanza Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na Sasa itakutana na USM Alger ya Algeria kwenye Fainali ya CAF Confederation Cup 2023.
Ikumbukwe Fainali za Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu 2023 zitapigwa nyumbani na Ugenini May 28 na June 3, huku Yanga akianzia nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam May 28 na mchezo wa pili utachezwa June 03 nchini Algeria.
Hii itakuwa Fainali ya kisasi kwa Young Africans, ikiwa na Kumbukumbu ya kukutana kwenye Michuano hii hatua ya Makundi mwaka 2018 na kufungwa mabao 4-0 nchini Algeria kabla ya Yanga kushinda 2-1 katika mchezo wa marudiano uliochezwa nchini Tanzania.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *